Thursday, October 29, 2020

MWAKINYO ATINGA BUNGENI, ATOA SIRI YA USHINDI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

Na RAMADHAN HASSAN – DODOMA


 

BONDIA Hassan Mwakinyo, ametambulishwa jana bungeni huku akisimulia jinsi alivyokopa fedha kwa rafiki yake ambayo ilimwezesha kucheza pambano lake nchini Uingereza.

Mwakinyo alishinda pambano la uzito wa super welter dhidi ya bondia Sam Egginton wa Uingereza, baada ya kumpiga kwa TKO katika raundi ya pili ya pambano hilo.

Pia wabunge wamepitisha kwa kauli moja kumchangia Sh 20,000 kila mmoja bondia huyo, ambapo jumla ya zaidi ya shilingi milioni 7 zilipatikana.

Akizungumza mara baada ya kutoka bungeni, Mwakinyo, alisema alikosa msaada wowote kuanzia maandalizi mpaka alipokwenda Uingereza kwa ajili ya pambano hilo.

Alisema hakuwa na meneja na alisafiri kama mkimbizi, lakini anashukuru ushindi aliopata umemfanya ajulikane.

“Nimesafiri kama mfungwa, nilikopa fedha kwa rafiki yangu leo kila mmoja anasema wakala wangu, nasema hapana sina meneja wala wakala.

“Sikuwa na msaada wa aina yoyote kuanzia maandalizi mpaka kwenda Uingereza nilikuwa kama mkimbizi, hata fedha za visa nilikopa kwa rafiki yangu ambaye ni mwanafunzi wa chuo ambaye alinikopesha Sh 200,000 zilizokuwa za ada,” alisema.

Mwakinyo alisema wakati akipanda ulingoni aliamini kwamba lazima atapata ushindi kutokana na mazoezi ya kutosha aliyofanya.

Bondia huyo alisema alikuwa akiamini hakuna ngumi isiyouma hivyo alijitahidi kuhakikisha zinampata mpinzani wake.

“Nilijiamini kwa mazoezi na niliamini hakuna ngumi isiyouma, hivyo nilikuwa nikirusha mfululizo,” alisema.

Alisema aliamini ipo siku atafanikiwa ndio maana aliweka hisia za ushindi mbele kabla ya kuanza kwa pambano hilo.

“Ukiamini unashinda ujue utashinda, mimi niliamini nitashinda na kweli nilishinda,” alisema.

Aidha, Mwakinyo, alitumia fursa hiyo kuwashukuru wabunge na Watanzania kwa kumpa heshima kubwa baada ya kurudi na ushindi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -