Tuesday, November 24, 2020

MWAMBUSI MENO YOTE 32 NJE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SALMA MPELI


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, ameonyesha meno 32 nje kufurahia  walichokifanya wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi MC Alger ya Algeria, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho barani  Afrika uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini  Dar es Salaam.

Mwambusi amesifu mabadiliko makubwa kwa wachezaji wake kwa kupanda kwa viwango vyao katika mchezo huo.

Akizungumza na BINGWA juzi, Mwambusi alisema viwango vya wachezaji wake vimebadilika mno na walicheza vizuri katika mchezo huo, ukilinganisha na walivyocheza michezo mingine.

Mwambusi alisema kutokana na uwezo wao, kuliwafanya kutengeneza nafasi nyingi, licha ya kwamba walishindwa kutulia na kuwa makini walipokuwa wanafika kwenye eneo la 18 na kufunga.

“Niwapongeze tu wachezaji wangu kwa kujituma zaidi na nikiri kuwa leo (juzi) walicheza kwenye kiwango cha hali ya juu sana na wameonyesha mabadiliko makubwa,” alisema Mwambusi.

Mwambusi alisema ni jambo zuri kupata ushindi nyumbani ili kujiwekea mazingira bora katika mchezo wa marudiano lakini ushindi huo ni mdogo, kwani itawafanya kuwa na kibarua kizito watakapokuwa ugenini.

“Tunashukuru kwa ushindi huo japo haujaturidhisha sana, kwani sote tunatambua ugumu uliopo kwenye viwanja vya ugenini na mara nyingi wanatufanyia mambo mengi hasa nje ya uwanja, lakini tunajiandaa na kukabiliana na changamoto zote ili tufanikiwe kusonga mbele,” alisema.

Alisema wanahitaji bao la mapema watakapokwenda kwenye mchezo wa marudiano ili kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -