Tuesday, December 1, 2020

MWAMBUSI: TUTAWAFUNGA ZANACO KWAO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA SALMA MPELI

KOCHA msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi, amesema wamewasoma wapinzani wao Zanaco na watawafunga katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga wanatarajia kurudiana na Zanaco Jumamosi wiki hii ugenini baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumzia matokeo hayo, Mwambusi alisema wameweza kuwafahamu vizuri wapinzani wao Zanaco baada ya mchezo huo na ana imani wataifunga nchini kwao na kusonga mbele.

Mwambusi alisema wamewasoma vizuri wapinzani wao na wanaamini wanaweza kuwafunga kwenye mchezo wa marudiano nyumbani kwao.

Alisema licha ya matokeo hayo kuwa kinyume na matarajio yao, lakini aliwapongeza wachezaji wake kwa kujituma ingawa wanakabiliwa na majeruhi wengi kutokana na kucheza mechi mfululizo.

“Wachezaji ni binadamu na miili yao si ya chuma, wamecheza mechi nyingi mfululizo, hivyo wamejizatiti kwa kiasi kikubwa kupambana lakini tumewaona wapinzani wetu na tumewajua, tunaamini kazi iliyobaki si ngumu sana,” alisema.

Alisema mpira hautabiriki, hivyo lolote linaweza kutokea kwenye mchezo wa marudiano na kuweza kuibuka na ushindi na kusonga mbele.

Katika hatua nyingine, winga wa Yanga, Simon Msuva, alisema alisema mpira una matokeo ya aina tatu, hivyo kutoka sare ni moja ya matokeo na haiwakatishi tamaa ya kufanya maandalizi zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -