Monday, November 23, 2020

MWAMKO WA KUIFANYA SANAA KUWA SEHEMU YA ELIMU BADO MDOGO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

SANAA ni kazi ya ubunifu ya mwanadamu yenye kuleta mvuto machoni na hisia zenye nguvu mwilini, ni tafsiri yangu tu, kwa mfano ungo wa kupetea mchele au maharage, msanii anaweza akabuni kitu kwenye huo ungo, mara tu ukageuka kuwa pambo badala ya chombo. Michoro mingi imesaidia kuelimisha jamii kuliko mwalimu darasani au mwalimu ataitumia michoro hiyo kumrahisishia kazi ya kufundishia kwa lugha nyepesi.

Angalia maeneo machache tu yanayotumia sanaa utagundua mafanikio makubwa, kwa mfano, kwenye harusi, mikutano ya siasa, makongamano, dhifa na ziara mbalimbali nje na ndani ya nchi nyuma ya mafanikio yake kuna sanaa. Wazee wetu walifanikiwa sana kuwa wenye hekima na busara, tukiachilia mbali kwamba walikuwa wanamuogopa Mungu, sanaa iliwasaidia sana, kwa mfano baada ya mavuno kutakuwa na ngoma, ndani ya ngoma kutakuwa na nyimbo, zile nyimbo zilikuwa zinabeba ujumbe mzito, ama wa kuonya au kushutumu au kufurahisha. Na matamasha hayo hufanyika mara nyingi kutokana na mavuno yalikuwaje kwa kipindi hicho.

Mwezi uliopita rafiki yangu mmoja  ambaye ni mkufunzi wa sanaa ya kudansi, alinitembeza pale Makumbusho ya Taifa ili nione ukumbi au jukwaa la kisasa la maonyesho. Kwa kweli ni jukwaa la kisasa kabisa, ila ugomvi wangu mimi ni kwamba je, linatumikaje na je panatangazwa ipasavyo ili watu wajue sasa kwamba eneo lile kuna maonyesho yanafanyika?

Nasema hivi kwa sababu  ni muda mrefu umepita sasa hapa Dar es Salaam bila kuwepo na ukumbi maalumu wa maonyesho. Hivyo watu wengi walikata tamaa na hawafahamu sasa ni wapi wanaweza kwenda kupata burudani. Ilikuwa ni vyema kwa wamiliki kutangaza kwa  nguvu zote juu ya uwepo wa ukumbi huo na maonyesho yanayofanyika  ili kurejesha hadhira ya maonyesho ya sanaa iliyopotea.

Kwa sasa kila mmoja ametingwa na mambo, mfano mtoto  wa shule ana msongo wa mawazo juu ya masomo yake, mwalimu ana msongo wa mawazo, mzazi ana msongo wa mawazo, kondakta wa basi ana msongo wa mawazo, muuza duka  halikadhalika, bosi kazini ana msongo wa mawazo, je hawa watu wakikutana wataongea nini?

Jambo moja tu ambalo naweza kukwambia ambalo watu huwa hawaamini, ni kwamba hatuna pa kwenda kuondoa msongo wa mawazo, maana si lazima kila mtu anapenda mpira na ukweli mpira hauwezi kutoa msongo kwa sababu timu yako unayoshangilia inaweza kufungwa, vipi hapo sasa?

Tiba sahihi ni sanaa za maonyesho, lazima sanaa za maonyesho zipewe kipaumbele kwa dunia ya sasa yenye mikanganyiko mingi, kama mtagundua wakati Ze Comedy inaanza, kulikuwa na foleni kwenye barabara watu wanawahi kutoa msongo wa mawazo.

Kule Afrika Kusini yuko kijana mmoja anaitwa Trevor Noah, Kenya yuko mchekeshaji, Erick Omondi, yupo Evans Bukuku, kidoogo na Steve Nyerere. Hawa watu wanaweza kukuondolea msongo wa mawazo lakini zipo ngoma na dansi, kuna watu wamerekebishwa tabia na michezo ya kuigiza tu, hadithi, nyimbo, mashairi.

Mwisho niwaombe wadau wa sanaa kupigania hili ili kujenga vijana na jamii kwa ujumla kupata mwamko mpya wa kupenda sanaa za jukwaani, kule kuna mafundisho mengi na michezo inatupa wasaa mzuri wa kutafakari mambo kwa upana wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -