Friday, December 4, 2020

MWANAMKE JITATHMINI, KISHA JIJUE WEWE NI WA AINA GANI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA RAMADHANI MASENGA,

KUNA tofauti kati ya mwanamke na mwanamke makini linapokuja suala la uamuzi katika mambo ya mahusiano. Mwanamke tu, kwa maana ya jinsia, yeye anaweza kutaka mwanamume mtanashati ama mwenye pesa ili awe mwandani wake. Ila mwanamke makini yeye huwa na vigezo tofauti. Kwake linapokuja suala la mahusiano akili na hisia zake humwongoza kumpata mtu sahihi wa maisha yake.

Mara nyingi nimewahi kusikia wanaume wakilalamika juu ya aina ya wanawake waliokuwa nao. Wanasema wanawake wao hata kabla ya ndoa wamegeuka kuwa mizigo mizito katika maisha yao kwa sababu ya mahitaji ya hovyo na tabia zao.

Mwanamke unakuta kila fasheni ya nguo anataka awe nayo, kila onesho la muziki anataka kuhudhuria. Huyu ni mwanamke mzigo kwa mawanamume makini.

Ikumbukwe, linapokuja suala la uhusiano wanaume hutofautiana sana. Mwanamume ambaye yupo kwa ajili ya kustarehe tu na mwanamke bila kuhitaji kuishi naye katika maisha makini ya ndoa, huenda asipende mwanamke mtulivu na mwenye kukwepa starehe.

Wao wanapenda sana wanawake micharuko kidogo, wenye kujua viwanja na pombe zote za mjini. Mwanamume mpenda starehe asiye na mipango mirefu na mwanamke, kuwa na binti wa aina hii kwake huwa ni furaha na raha sana.

Ila kuna kundi la wanaume wengine. Wao muda mwingi wanapokuwa na wapenzi wao huzungumzia namna ya kutengeneza nao familia ya furaha, heshima na maadili. Mara nyingi hutumia muda wao kukanyana na kutakiana kila la kheri katika matendo na maamuzi yao.

Kwa mwanamke mjinga, mwenye pupa ya maamuzi, mwanamume huyu anaweza kumuita mkoloni kisa tu anamkataza kwenda club ama kujumuika na kundi la marafiki wa hovyo.

Nimeona wanawake wengi wakiachana na watu wa aina hii na kukimbilia kwa wanaume ambao watawapa nafasi ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya. Kitu wasichojua ni kuwa, wale wenye kujidai kutoa uhuru mpana huwa si watu makini katika maisha yao, ndiyo maana hawajali hata wakiona wahusika wakipotea.

Wewe binti, mwanamume wako yuko vipi? Umemsoma na kugundua ana malengo gani na wewe? Uhuru wako kwake uko vipi? Usipende kuchekelea uhuru anaokupa bila kujua sababu yake. Mingine ni mitego.

Siyo vema mwanamume kumbana sana mpenzi wake katika mahusiano, ila ni vema mwanamume akamwelekeza mpenzi wake mipaka ya matendo, marafiki na hata maneno yake. Kufanya hivi maana yake mhusika anataka kumfanya mwanamke wake atoshe katika vigezo vyake na asitamani mwanamke mwingine.

Wanawake wengi wanakosea kuwa viburi kwa watu wao pindi wanaporekebishwa. Kitendo hiki kinakuja kuwagharimu baadaye kwa sababu wahusika baada ya kuona wanawarekebisha wakina fulani na wao hawaelekei basi huamua kupeleka macho kwa wengine wenye kuonekana kukubaliana na misimamo yao ya kimaisha. Baadaye unakuta mwanamke kutoka katika mahusinao haya anasema wanaume wabaya, eti alimuahidi kumuoa na sasa kamkimbia.

Ndiyo alikupenda na hata kukuahidi kukuoa. Ila atakuoa vipi ikiwa alisema hataki uwe na kundi la marafiki wa hovyo na wewe hukusikia? Atakuoa vipi ikiwa alikwambia aina ya mavazi unayovaa yanamvunjia heshima na ni kinyume na msimamo wake wa kiimani ila wewe hukusikia? Mara nyingi wanawake wanalalamika bila kujua chanzo cha mateso yao katika mahusiano yamezalishwa na wao.

Ili mwanamke umfanye mwanamume wako akufikirie kila muda  na kutamani kukuoa, inabidi umfanye ajihisi maalumu kwa matendo na maneno yako. Inabidi utekeleze mengi ya matakwa yake ili asipatwe na tamaa ya kwenda nje.

Kuna binti mmoja alikuwa na mpenzi ambaye anapenda sana wanawake wenye kujisitiri. Mpenzi wake huyo alipomwambia kuwa na yeye abadilike kimavazi, kutoka katika mavazi ya ‘kimjini mjini’ mpaka katika mavazi ya staha na heshima, alikataa kwa kusema kuwa yeye amezoea hivyo na amekulia katika mavazi hayo.

Mwaka mmoja baadaye, mwanamume wake akabadilika tabia. Badala ya kuwa anamsisitizia avae mavazi ya kujisitiri akawa anamwamcha tu. Mara akawa pia hamtafuti tena kwenye simu.

Mwezi uliopita yule binti alipatwa na mshtuko na kuzimia baada ya kusikia yule mwanamume wake ameoa kimya kimya binti fulani mpole kutoka Tabora, mwenye kujisitiri na mcha Mungu. Kuwa makini.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -