Thursday, December 3, 2020

MWANDAMI : WADAU SINGIDA UNITED MJIANDAE KUNUNUA HISA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA NATHANIEL LIMU, SINGIDA

MKURUGENZI wa klabu ya Singida United, Yusuph Mwandami, ametoa wito kwa wakazi wa Singida na wadau wengine kujiandaa mapema kwa ajili ya kununua hisa pindi taratibu zote zitakapokamilika za kuiwezesha klabu  hiyo kuwa kampuni.

Akizungumza na BINGWA ofisini kwake jana, Mwandami, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (CCM) Mkoa wa Singida, alisema ili Singida United iweze kujiendeleza kwa ufanisi zaidi, inahitaji iwe na uwezo mzuri kiuchumi.

Alisema kwa sasa Singida United ilipofika, haiwezi kuendelezwa na yeye binafsi wala na wadau wachache waliopo.

“Tukipata wadau na wananchi wengi wakajitokeza kwa dhati kununua hisa, nina uhakika Singida United itashiriki ligi kuu bila shida yo yote. Pia wachezaji watapata huduma zao zote stahiki bila shida na kwa wakati,” alisema Mwandami, ambaye pia ni mchimba madini.

Mwandami alitumia  fursa hiyo kuwapongeza baadhi ya wadau na wananchi kwa ujumla, kwa michango yao   ya hali na mali, iliyowezesha Singida United kufika hapo ilipo.

“Kwa kweli baadhi ya wananchi wamejitolea fedha zao na hata ‘kelele’ uwanjani nazo zimekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio haya. Asanteni sana na tuongeze ushirikiano zaidi pamoja na kununua hisa ili timu isonge mbele zaidi kuutangaza mkoa na taifa kwa ujumla,” alisema.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo alisema taratibu zinaendelea kufanywa kwa ajili ya kuandaa sherehe kabambe ya kuipongeza timu kwa mafanikio yake.

Alisema sherehe hiyo itapambwa na mchezo wa kirafiki kati ya Singida United na Simba au Yanga za jijini Dar es Salaam. Baada ya taratibu zote za sherehe hiyo kukamilika, siku ya sherehe itatangazwa rasmi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -