Wednesday, October 28, 2020

MWANZA UCHAGUZI UMEKWISHA PIGENI KAZI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

MWISHONI mwa wiki iliyopita Chama cha Soka Mkoa Mwanza (MZFA), kilifanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wao wapya watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka minne ijayo ya kuletea maendeleo ya soka mkoani humo.

Katika uchaguzi huo, Vedastus Lufano amepewa dhamana ya kuwa Mwenyekiti mpya wa MZFA baada ya kumbwaga Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Wilaya ya Ilemela (MNEC), Israel Mtambalike.Lufano alipata kura 20 dhidi ya 14 za Mtambalike katika uchaguzi huo.

Ni wazi kuwa wajumbe waliopata nafasi  ya kupiga kura katika uchaguzi huo walitumia haki yao ya msingi kikatiba na kuchagua viongozi ambao wanaona wanawafaa kuliokoa  jahazi la Mwanza na kuwapa maendeleo katika nyanja ya mchezo wa soka unaopendwa na watu wengi zaidi duniani.

Uchaguzi umekwisha yaliyopita si ndwele tugange yajayo, kitu kimoja ninachotaka kuwaambia viongozi hao wapya kuwa watumie madaraka yao vizuri na kuwaletea maendeleo makubwa watu wa Mwanza katika mpira wa miguu.

Mwanza ni moja kati ya mikoa michache iliyowahi kusifika kwa kutoa vipaji vya wachezaji na timu zilizoleta ushindani mkubwa katika soka la Tanzania, hivyo wana imani kubwa kwamba uongozi mpya utahakikisha wanarejesha tena makali ya mkoa huo.

Mkoa wa Mwanza sasa hivi una timu mbili ambazo ni Toto Africans na Mbao FC, timu hizi zimekuwa hazifanyi vizuri katika michuano ya  Ligi Kuu Tanzania Bara, moja ya kazi kubwa mlionayo viongozi wapya kwanza ni kuhakikisha mnafanya kila linalowezekana kuzibakisha timu hizi mbili kwenye ligi ya msimu ujao.

Lakini kazi nyingine ambayo wanayo viongozi hawa ni kuhakikisha wanapandisha timu nyingine ikiwemo Pamba ambayo ilikuwa ni moja kati ya timu iliyoleta upinzani mkubwa kwa vigogo wa soka hapa nchini Simba na Yanga.

Sote tunajua sifa ya timu hii lakini leo hii ukienda Mwanza ukiuliza kuhusu Pamba, hakuna majibu sahihi utakayopewa kutoka kwa wadau wa mpira mkoani humo na wengine watakwambia timu hiyo ipo mifukoni mwa wanachama na haina hata ofisi.

Kwa hiyo viongozi wapya wa mkoa ni wajibu wenu sasa kufanya kazi ya ziada kuirejesha heshima ya soka la Mkoa wa Mwanza. Uwanja wa Nyamagana unafanyiwa matengenezo makubwa na utakuwa wa kisasa muda si mrefu, lakini mnao uwanja wa CCM Kirumba ambao unamilikiwa na CCM; moja ya viwanja bora kabisa na vikubwa kwa Tanzania.

Itakuwa aibu mji wenye viwanja viwili vizuri unakuwa na timu dhaifu kabisa katika ligi kuu au unakosa timu za ligi kuu. Ninaamini maneno yenu mazuri ya ahadi kwa wajumbe juu ya kuinua soka la Mwanza ndiyo yamewapa nafasi ya kupewa kura nyingi, hivyo ni vyema mkatekeleza ahadi zenu.

Jambo jingine kwa wadau wa soka wa Mwanza ni kwamba sasa uchaguzi umekwisha. Ni vyema mkazika tofauti zenu na makundi yenu ya uchaguzi na kuhakikisha mnashirikiana na wadau, vyama vya soka vya wilaya saba vya mkoa huo kuhakikisha  vinapiga hatua na kuzisaidia timu za Toto Africans, Mbao FC, Alliance Academy na Pamba FC zinauletea sifa mkoa huo.

Jambo jingine mnatakiwa  kuhakikisha wanawaunganisha wadau wa soka wakiwemo viongozi wa Serikali na vyama vya siasa, taasisi, mashirika, kampuni za watu binafsi ili kuwa na umoja utakaowezesha soka la Mkoa wa Mwanza kurejea katika hali yake ikiwemo kutoa wachezaji wengi kujiunga na timu za Taifa Stars, Serengeti Boys na Twiga Stars.

Kila mmoja kwa nafasi yake akiguswa na kuendeleza soka kuanzia ngazi ya kata, wilaya na mkoa itasaidia vijana wengi kujitokeza kucheza mpira, pia hakikisheni  kila wilaya kunachezwa ligi tena ligi zenye ushindani wa haki ili kupata timu bora zaidi kwenye mashindano yanayouwakilisha Mkoa wa Mwanza katika ngazi ya taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -