Wednesday, November 25, 2020

MWIGULU KUIANDALIA UBINGWA SINGIDA UTD

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA
MBUNGE wa Jimbo la Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba, amesema Siginda United itachukua ubingwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA mjini hapa, Mwigulu alisema ameweka malengo ya kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa msimu ujao.

Mwigulu ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, alisema atahakikisha anazipiku Simba na Yanga kwa kufanya usajili wa kueleweka wa wachezaji.

Alisema timu hiyo itasajili wachezaji watano wa kigeni na kocha ambaye atasaidiana na Fred Minziro kuhakikisha ubingwa unatua Singida United.

“Nani amekwambia mimi Yanga damu, hilo hapana mimi ni Singida United tena siku hizi tuna jina jipya tunaitwa ‘The Wind Power’ kutokana na ule upepo wa umeme ambao haupatikani eneo lolote Tanzania,” alisema.

Mwigulu alisema kwa sasa wapo katika marekebisho makubwa ya Uwanja wa Namfua ili uweze kutumika kwa mechi za Ligi Kuu Bara.

Alisema timu hiyo itatumia jezi zenye rangi ya mmea wa alizeti ili kuonyesha zao linalopatikana katika mkoa huo.

Mwigulu alisema timu hiyo itavaa jezi nyeupe na nyumbani watavaa jezi yenye rangi ya jani la alizeti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -