Saturday, October 31, 2020

MZIMU WA MADRID WAZIDI KUMTAFUNA RONALDO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

ROME, Italia


STRAIKA mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amezidi kuandamwa na mzimu wa kuitema timu yake ya zamani Real Madrid, baada ya kushindwa kuziona tena nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Italia, Serie A.

Ronaldo aliondoka kapa tena uwanjani juzi katika mchezo ambao timu yake iliondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya 2-1 Parma na hivyo kuongeza idadi ya kushindwa kupachika bao kufikia mechi tatu tangu ajiunge na klabu hiyo.

Mkosi huo wa kushindwa kuondoka na bao uwanjani umekuja pia zikiwa ni siku chache, tangu apigwe chini katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora Ulaya, UEFA na aliyekuwa staa mwenzake Real Madrid, Luka Modric.

Ronaldo aliondoka Madrid baada ya kumalizika msimu uliopita na kwenda kujiunga na mabingwa hao wa Ligi ya  Serie A kwa ada ya Euro milioni  112, lakini mpaka sasa ameshindwa kupenya katika kuta za timu ambazo zinacheza soka la kukaba.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Ronaldo kushindwa kufunga mabao katika mechi tatu za kwanza za ligi kwani hali hiyo ilimtokea pia mwaka jana katika michuano ya La Liga, lakini baadaye akaweza kufunga mabao  26 katika mechi  27 aliwachezea mabingwa hao wa  Ulaya.

Hali hiyo pia ilimtokea mwaka mmoja uliokuwa umepita kabla ya msimu uliopita, lakini akaweza kuifungia mabao mengi Madrid katika mashindano mengine.

Katika kikosi cha Juve, Ronaldo ndiye ameshapiga mashuti mengi  kuliko mchezaji yeyote akiwa na 23 na ndiye ameshacheza dakika zote 270.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -