Saturday, November 28, 2020

MZUNGUKO WA PILI VPL UJE NA SOKA LA KITABU

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na HASSAN DAUDI,

HATIMAYE kile kivumbi cha mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) kinatarajiwa kuanza leo, ambapo viwanja mbalimbali vitawaka moto.

Hata hivyo, kwa miaka mingi, mashabiki wa soka hapa nchini wamekuwa wakidhulumiwa, timu zao haziwatendei haki hata kidogo.

Utafiti wangu mdogo umebaini kwamba, asilimia 80 ya mashabiki wanaoingia uwanjani kuangalia mechi za Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) huwa wamelipa fedha za kiingilio kufuata matokeo na si burudani ya soka.

Huwa wanapoteza muda tu kwenda viwanjani na badala yake wangeweza kufanya mambo mengine na kusubiri kusikia matokeo kupitia vyombo vya habari.

Ndiyo, mara nyingi wanapotoka uwanjani kutazama mchezo wa VPL, wanaambulia matokeo tu na si starehe iliyopo kwenye soka. Kiufupi, mashabiki wa soka la bongo hawaijui ladha ya soka la kuvutia kutoka kwenye timu zao.

Kwa maana nyingine, fedha wanazolipa milangoni ni kubwa kuliko kile wanachokikuta uwanjani. Inauma kuuziwa matokeo kwa Sh 5,000, hasa kwa kipindi hiki ambacho gharama za maisha ziko juu.

Wapo walioamua kulipa kisogo soka la Bongo na kuamua kuwa mashabiki wa klabu za Ulaya, hasa zile za Ligi Kuu England.

Siwaungi mkono hata kidogo, ila ninapohudhuria mechi za VPL ndipo ninapogundua kuwa wana kila sababu ya kufanya hivyo.

Aina ya uchezaji wa timu zetu haivutiii na hapo ndipo ninapoamini kuwa mashabiki wa soka la Bongo hawatendewi haki na timu wanazozishabikia.

Si tu katika mzunguko wa kwanza wa VPL msimu huu wa 2016-17, imekuwa hivyo miaka nenda-rudi.

Ni nadra kuona timu ikimiliki mpira japo kwa dakika tano bila kupoteza na kama itafanya hivyo, basi ni pale wanapokuwa kwenye lango lao.

Lakini pia, ni ngumu kuona bao linavyotafutwa kabla ya kufungwa. Mashabiki wanaokuwa uwanjani hawaoni mipango ya timu katika kusaka bao, ni vurugu tupu.

Utashangaa tu mpira umebutuliwa na mlinzi wa kati na kumkuta mfungaji ambaye pia huenda ameotea, lakini mwamuzi akapeta.

Tusikatae, hayo ndiyo aina ya mabao tunayoyashangilia kila tunapokwenda viwanjani kutazama mechi za VPL.

Tatizo ni makocha kushindwa kufundisha soka la kitabu, au ni wachezaji kutofuata maelekezo ya benchi la ufundi? Hapo sijajua.

Hali imekuwa mbaya zaidi kwa sisi tunaozipenda timu vigogo. Ni matokeo tu ndiyo yanayotufanya tuendelee kuzipenda na si soka la uhakika uwanjani.

Yanga, Simba na Azam, zote zina makocha wa kimataifa, lakini bado uwanjani ni majanga matupu.

Japo nimekuwa mhudhuriaji mzuri wa mechi za VPL, wala sikumbuki ni lini Yanga, Simba na Azam ziliwahi kucheza kwa kiwango cha hadhi yao.

Watakavyocheza leo watakufurahisha, lakini ukiwatazama baada ya wiki mbili utabaki na mshangao, hasa ikizingatiwa kuwa hizo ndizo timu kubwa hapa nchini kwa sasa.

Kutokana na ukubwa wa jina lake hapa nchini na Afrika kwa ujumla, inapaswa kuwa jambo la kushangaza kuiona Yanga ikipiga pasi 15 bila kupoteza mpira?

Natamani kuona mzunguko wa pili ukija na mapinduzi ya soka la uwanjani kwa klabu zetu.

Ni wakati mwafaka sasa kwa wachezaji na makocha wa timu za VPL kuamka na kufikiria juu ya kuwatendea haki mashabiki wao.

Mbali na matokeo, mashabiki wanahitaji burudani ya mchezo wa soka ambayo wamekuwa wakiishuhudia kwenye ligi za barani Ulaya.

Kama makocha na wachezaji watatekeleza wajibu wao ipasavyo, naamini tutashuhudia mapinduzi makubwa ya soka la kisasa katika mzunguko wa pili unaoanza leo.

Gwiji la soka la Brazil, Pele, aliwahi kusema mabao ndiyo kila kitu katika mchezo wa soka.

Huenda alikuwa sahihi kwa upande mmoja, lakini alisahau kuwa kandanda ni zaidi ya kuibuka na ushindi.

Naamini hakutambua au alipuuzia burudani inayopatikana kwenye mchezo huo unaopendwa zaidi duniani.

Lazima bao lipatikane katika hali itakayomvutia mtazamaji, hicho ndicho Pele alichokisahau.

Hivi unajua kwanini Ronaldinho ‘Gaucho’ anakumbukwa zaidi kuliko Rud van Nistelrooy wakati hakufikia hata nusu ya uwezo wa kupachika mabao wa Mholanzi huyo?

Van Nistelrooy alikuwa mfungaji hatari, lakini aina yake ya ufungaji haikuwa ya kuvutia na ndiyo maana si rahisi kukumbuka mabao yake 10 akiwa Old Trafford.

Kwa upande wake, Gaucho alikuwa mburudishaji. Aliufanya mchezo wa soka uonekane rahisi hata kwa sisi tusio na vipaji.

Alifunga mabao kwa ‘style’ ambayo ingemfurahisha hata adui yake. Ni rahisi kukumbuka mabao yake hata yale ya miaka 10 iliyopita.

Pele anaamini mabao ndiyo kila kitu, lakini utamu wa soka ni pale yanapopatikana kwa njia ambayo itatufanya tutazamane na kutabasamu. Ni hayo tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -