Thursday, December 3, 2020

NAHODHA KAGERA AVUJISHA SIRI ZA MEXIME

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA WINFRIDA MTOI,

NAHODHA wa Kagera Sugar, George Kavila, amevujisha siri za kufanya vema  katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Kavila alisema mafanikio hayo yanatokana na mfumo wa ufundishaji anaoutumia kocha mkuu wao, Mecky Mexime.

Kavila alisema wamekuwa wakifanya vizuri tofauti na msimu uliopita walionusurika kushuka daraja kabla ya ujio wa Mexime katika kikosi hicho.

Alisema Mexime anajua jinsi ya kuwalea wachezaji na kuwaandaa kwa mapambano tofauti na makocha wengine waliomtangulia.

“Ni kweli tangu amefika Mexime kikosi chetu kimeimarika kutokana na kujua wakati wa kumfanyisha mazoezi mchezaji na kuelewa bila kutumia nguvu huku akitoa muda mwingi wa mapumziko, kitendo kinachowafanya wawe na hamu ya kucheza mechi muda wote,” alisema Kavila.

Alisema mazoezi ya soka ni yale yale yanayotolewa na makocha wengine, lakini kuna mbinu nyingine anazotoa na kumfanya mchezaji afurahie mchezo.

“Kipindi cha nyuma tulikuwa tunafanya mazoezi muda mrefu na matokeo bado yalikuwa hayaridhishi, lakini hivi sasa muda mfupi na kila mchezaji anashika kile anachoelekezwa.

Nahodha huyo alisema kitu kingine kinachochangia timu yao kufanya vizuri ni uwepo wa wachezaji wengi vijana na wale waliosajiliwa kuongeza nguvu.

Kagera Sugar inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 36, ikiwa imecheza mechi 23, imeshinda 11, sare sita na kupoteza sita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -