Sunday, November 29, 2020

NAKATAA UNAFIKI WA TFF KUMUUNGA MKONO MAKONDA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

VITA ya kupambana na dawa za kulevya inaendelea. Wafanyabiashara maarufu, wanasiasa, wasanii na watu wengine wa kawaida wanakwenda polisi kuhojiwa kutokana na tuhuma za kuhusika na biashara na matumizi ya dawa hizo.

Hii ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuanza kuwataja wasanii akiwemo Wema Sepetu na baadaye wanasiasa kama Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan na wafanyabiashara wakubwa hapa nchini.

Ilikuwa ni awamu ya pili kwa mkuu wa mkoa, Makonda kuendelea kuwataja watu waliodhaniwa kujihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya na tayari wengine wamefika polisi na kuhojiwa.

Lakini baadhi ya watu waliohojiwa tayari wamefikishwa mahakamani ili kujitetea  baada ya kutuhumiwa kuhusishwa na  biashara na matumizi ya dawa hizo, wengine wakiwa wamehojiwa na kuachiwa, lakini wakitakiwa kuendelea kuripoti polisi huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea.

Ni juzi tu tuliposikia mrembo anayejihusisha na kazi za kupamba video za muziki nchini (video queen), Agness Gerald maarufu kwa jina la Masogange kuwa alikuwa anashikiliwa na Jeshi la  Polisi Kanda Maalumu  ya Dar es Salaam.

Ilidaiwa Masogange ni mmoja wa watu ambao wanatuhumiwa kuhusika na biashara hizo, licha ya kwamba  haijathibitika moja kwa moja kama ni kweli ndio maana zimebaki ni tuhuma dhidi yake.

Ni safari ndefu ambayo mkuu wa mkoa  Makonda ameanzisha, kwani kabla ya Masogange kudaiwa kushikiliwa na polisi nilitarajia kusikia kutajwa orodha ya awamu ya tatu.

Nilikuwa nimetega sikio nikisubiri pengine angeweza kutajwa kigogo mzito ama katika Serikali au mfanyabiashara mwingine mkubwa kwa kuwa hao ndio wenye mitaji mikubwa ya kufanya biashara hizo.

Sikushtuka sana katika orodha hizo kama wangetajwa vijana wanaotumia dawa za kulevya kwa sababu tunawaona wengi mitaani jinsi walivyoathirika.

Ni kundi kubwa la vijana wameathirika kwa kutumia dawa za kulevya, lakini maisha yao yapo hatarini na inadaiwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakiingiza dawa hizo nchini kutoka nchi nyingine.

Lakini inadaiwa baadhi ya vijana wamekuwa wakitumiwa kubebeshwa mizigo ya dawa za kulevya kuingia nchini.

Binafsi naunga mkono juhudi za Makonda kwa kuanzisha vita dhidi ya dawa za kulevya  kwa mkoa wake, lakini  ikilenga nchi nzima kwani kila pembe ya nchi kunadaiwa kuwepo kwa watumiaji wa dawa hizo.

Makonda umefanya kazi nzuri hadi hapo ulipofikia, lakini umeninyima fursa ya kukusikia ukiwataja wachezaji wa soka ambao wanahusika na biashara ya dawa za kulevya.

Nilitarajia hili kwa Makonda kuwa  katika orodha mojawapo ya watu wanaodaiwa kutumia dawa ya kulevya ningesikia kutajwa kwa  jina na mchezaji maarufu wa soka anahusika na biashara au matumizi ya dawa za kulevya.

Pamoja na kwamba vita yake ya kupambana na dawa za kulevya inaendelea, si wasanii pekee ambao wanadaiwa kutumia dawa za kulevya na wanasoka wanaweza kuwepo.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF), lenyewe lipo mbele ya Makonda katika kupambana na vita ya dawa za kulevya, kwani katika mashindano yake ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, linakuwa makini kufanya uchunguzi kwa wachezaji wanaowahisi kutumia dawa za kuongeza nguvu mchezoni.

Katika michuano hiyo, shirikisho hilo lina kawaida ya kuwafanyia vipimo wachezaji au mchezaji wanayemtilia shaka kama anatumia dawa za kulevya, kwa kupima baada ya kumalizika kwa mchezo ili kujiridhisha.

Huu ni utaratibu wa CAF, lakini Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lenyewe halima utaratibu wa kuwapima wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, daraja la kwanza au madaraja mengine ya chini.

Kungekuwa na utaratibu huo, tungeweza kusema kwamba wanasoka hawamo kwenye tuhuma za biashara na matumizi ya dawa za kulevya, kwani baadhi ya wachezaji waliwahi kutuhumiwa na kuhusika.

Nitakataa unafiki wa viongozi wa TFF wa kumuunga mkono Makonda wa kumsaidia kupambana na vita ya dawa za kulevya, wakati hawajaonyesha mfano kwa wachezaji wanaoshiriki ligi zao kuchukuliwa vipimo kama ambayo wanavyofanya CAF kila mwaka katika mashindano yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -