Wednesday, November 25, 2020

NAMBA ZILIVYOMHUKUMU RANIERI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LEICESTER, England

MIEZI tisa baada ya kubeba taji la Premier League akiwa na Leicester City, Claudio Ranieri, ametimuliwa. Kwanini? Namba hazisomi kabisa msimu huu!

Muitaliano huyu ametimuliwa klabuni hapo saa 24 baada ya Leicester kupokea kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Sevilla kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hii si Leicester ile iliyofahamika na kupendwa na wengi msimu uliopita, nini kimebadilika? Takwimu zinatupa majibu sahihi zaidi kwanini mabosi wa Leicester wamechukua uamuzi huo mgumu wa kumtimua ‘Mr Tinkerman’.

32 – Mpaka wakati kama huu msimu uliopita, Leicester walikuwa na pointi 53 kwenye msimamo wa EPL, lakini safari hii wana pointi 21. Tofauti ya alama 32!

14 – Msimu huu wameshachezea vichapo 14, kwenye ligi tofauti na msimu uliopita walifungwa mechi mbili, usisahau kwenye mechi 25 walizocheza mpaka sasa, wameshinda tano tu.

24 – Uwezo wao wa kufunga ni tatizo pia msimu huu. Mpaka sasa wamepachika mabao 24 tu ukilinganisha na mabao 47 waliyofunga baada ya mechi 25 msimu uliopita.

0 – Aisee, ni ngumu kuamini lakini ukweli ni kuwa Leicester hawajashinda mchezo wowote ugenini. Kwenye michezo 13 waliyocheza ugenini wamepata sare tatu tu, hii ni rekodi mbaya zaidi kuwekwa kwenye Premier League.

0 – Hii hapa kali nyingine. Tangu mwaka 2017 uingie Leicester hawajafunga bao lolote kwenye Premier League. Kwenye mechi sita, wamepata pointi moja tu, kwenye mchezo waliopata matokeo ya 0-0.

11 – Msimu huu wamepata sare kwenye mechi 11, ni tofauti na msimu uliopita walipopata sare tatu tu kwa michezo yote mpaka wanabeba taji.

3.2 – Wastani wa Leicester kupiga mashuti msimu huu, ni timu tatu tu zenye wastani huu wa chini. Msimu uliopita, walishika nafasi ya tano kwa wastani mzuri wa kupiga mashuti langoni.

343 – Dakika ambazo Leicester waliongoza mchezo kwa kupata bao, ni tofauti na msimu uliopita walipokuwa na wastani wa dakika 863 kwa kupata bao la kuongoza.

5 – Straika wa England, Jamie Vardy, aliyefunga mabao 11 mfululizo kwenye jumla ya mabao 24 na kucheza fainali za Euro 2016, amefunga mabao matano tu msimu huu.

17/11 – Mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, Riyad Mahrez, akiwa na rekodi nzuri ya kufunga na kuasisti, amefunga mabao matatu tu na kutoa asisti mbili mpaka sasa.

1 – Danny Drinkwater ametoa asisti moja tu msimu huu, tofauti na msimu uliopita akitoa asisti saba.

5/3 – Straika aliyesajiliwa msimu huu, Islam Slimani, ametoa asisti tatu na kufunga mabao matano, akishirikiana na Jamie Vardy kwenye safu ya ushambuliaji.

86 – N’Golo Kante, mmoja kati ya wachezaji bora waliotoa mchango mkubwa msimu uliopita, amefanya ‘takles’ 86 kwenye mechi 24 alizocheza akiwa na jezi ya Chelsea msimu huu, akishika nafasi ya tatu kwenye Premier League, nyuma ya Daniel Amartey, Wilfred Ndidi na Nampalys Mendy.

Tangu aondoke Leicester, sehemu ya kiungo ya klabu hiyo imeyumba na imekuwa ikiruhusu timu kushambuliwa mara kwa mara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -