Wednesday, November 25, 2020

NAMSHANGAA ZINEDINE ZIDANE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Markus Mpangala

MCHEZAJI yeyote anayesajiliwa na Real Madrid huwa anapewa kijitabu cha mwongozo. Kitabu hicho kinajulikana kwa jina la Etiquette.

Kanuni za kitabuni zinasema mchezaji yeyote wa Madrid hatakiwi kumzonga mwamuzi ili atendewe haki katika mchezo.

Kinaeleza kuwa, hakuna ufahari wowote kwa mchezaji wa Real Madrid kumshinikiza mwamuzi au matendo yoyote yenye kuashiria kumfanyia fujo au kumwondolea utimamu wake katika mchezo.

Si makipa wala mabeki. Si mawinga wala viungo. Si washambuliaji wala wachezaji wa akiba. Si Galactico wala Castilla. Wote wanatakiwa kufuata mwongozo huo. Mchezaji akitoka Castilla, kwa mfano Mariano Diaz au Tejero, wakicheza timu ya wakubwa kanuni ni ileile.

Castilla kule kanuni ni ileile. Hukuti wakimlalamikia mwamuzi wa mchezo. Etiquette inafanya kazi yake ipasavyo kwa kila ngazi ya wachezaji wa Real Madrid.

Shabiki wa Madrid huku kwetu Tanzania ambaye hana uwezo wa kufika Santiago Bernabeu anaweza kupata masimulizi ya Etiquette kupitia kitabu cha “The Real Madrid Way:  How Values Created the Most Successful Sports Team on the Planet kilichoandikwa na mwandishi Steven G. Mandis.

Etiquette ndio msingi unaowafanya wachezaji wetu wawe na adabu, nidhamu, staha, utulivu na mambo yote mazuri kuhusu timu, hasa kutwaa mataji.

Kwamba timu inaamini mbinu za ushindi ni pamoja na kumheshimu mwamuzi na kumwachia jukumu lake la kuamua mechi katika uwanja wowote wanaocheza.

Sasa kwa wachezaji hilo linafahamika. Ni moja ya mambo yanayosisimua, kwani yanawafanya wachezaji wawe na adabu kila dakika wanayokuwa uwanjani. Ni sababu hiyo huwezi kuwakuta wachezaji wetu wakilalama lalama kwa mwamuzi.

Huwezi kukutana na hila za kushinikiza mwamuzi achukue maamuzi ya kuwapendelea. Badala yake mwamuzi ataamua mwenyewe. Hiyo ndiyo Real Madrid ninayoijua. Hiyo ndiyo Etiquette ninayohusudu.

Hakuna kitu kinachonishangaza kwa kocha wetu Zidane tangu alipokuwa msaidizi wa Ancelotti. Kwa wachezaji wanaonekana kumezwa na haiba yake vizuri sana. Wanamhusudu kama kocha.

Wanamhusudu kama mchezaji aliyetikisa ulimwengu. Wanamhusudu kama mwanadamu, mkimya asiye na mbwembwe na mwingi wa kuficha siri zake.

Zidane ni mwingi wa kuficha fikra zake. Hasemi mara kwa mara. Hatengenezi habari binafsi. Hatengenezi habari binafsi kwa timu. Bali anatengeneza kutokana na timu.

Kwa muda mrefu nimemfuatilia Zidane, lakini sikuwahi kumwona akimlalamikia mwamuzi kwa uamuzi wowote kwenye uwanja wowote tunaocheza hata ikionewa.

Hivi majuzi alisema kuwa, Real Madrid haina mpango wa kutegemea kubebwa na waamuzi, bali wachezaji wanafanya kazi yao.

Zidane yuko hivyo tangu zamani akiwa mchezaji. Kila siku mechi ikiendelea yeye hana muda wa kumwangalia mwamuzi wa akiba, mshika kibendera kwa nia ya kupendelewa.

Yaani si kocha wa kulalama lalama na kuwashawishi waamuzi wampendelee. Tazama muda wote anaokuwa kwenye benchi.

Tazama miondoko yake anapokuwa kwenye eneo la kocha ndani ya uwanja wowote duniani. Tazama anapozungumzia mchezo uliochezwa au kabla ya kuchezwa kwenye vyumba vya mikutano na vyombo vya habari.

Kuna makocha ambao mara zote wamekuwa wakiwashutumu marefa. Wakati wa Jose Mourinho akiwa Real Madrid ilikuwa jambo la kawaida kuona akiwashutumu marefa wakati mchezo unapoendelea.

Lakini najiuliza, huyu Zidane kwanini huwa halalamiki hata pale Madrid inapoonewa dhahiri? Huwa najiuliza kwanini kocha wetu hana muda wa kuwafokea waamuzi kutokana na makosa yao dhidi ya timu yake?

Najiuliza kwanini hawafokei waamuzi wa akiba? Kwanini hana muda wa kuzungumza na waamuzi? Mara nyingi yeye akitoka kwenye eneo la kocha na kurudi benchini basi anakwenda kuzungumza na David Bettoni.

Akimfuata Bettoni basi anakwenda kuzungumza masuala ya mbinu za mchezo na mabadiliko yake. Huyo ndiye Zidane. Huyo ndiye kocha wa timu maridadi kuwahi kutokea ulimwenguni.

Huyu ndiye kocha mwenye utulivu na mchoyo wa maneno. Huyu ndiye kocha ambaye mwamuzi anatakiwa kutafakari mwenyewe juu yake.

Sijawahi kuona Zidane akipewa adhabu ya kuondolewa kwenye benchi kwa kukorofishana na waamuzi. Hakuna siku hata moja tangu alipokuwa kocha msaidizi hadi kocha mkuu.

Zidane ni Zidane tu. Matendo na mwenendo wake vinahamasisha wachezaji kucheza vema, kumpigania na kumpenda zaidi kila kukicha. Halla Madrid!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -