Tuesday, November 24, 2020

NANI AMEFUNGA BAO KALI ZAIDI KATI YA MKHITARYAN NA GIROUD?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England


MJADALA mkubwa unaosumbua vichwa vya mashabiki wa soka duniani ni ule wa mabao yaliyofungwa na straika wa Arsenal, Olivier Giroud na kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan.

Mkhitaryan aliteka vichwa vya habari siku ya ‘Boxing Day’ kwa bao alilofunga kwa mtindo wa nge ‘Scorpion’ dhidi ya Sunderland katika dimba la Old Trafford, lakini siku sita baadaye, Giroud alifunga kwa mtindo huo huo katika pambano la Arsenal dhidi ya Crystal Palace.

Lipi ni bao kali katika hayo mawili? Ni lile la Mkhitaryan au la Mfaransa, Olivier Giroud? Mpaka sasa dunia imeshindwa kupata jibu sahihi katika mjadala huu.

Wote wawili walifunga wakiwa ndani ya eneo la 18 lakini tofauti yao ni mbili tu, kwanza Mkhitaryan alifunga mpira ukiwa chini kidogo huku Giroud akifunga mpira ukiwa juu.

Pia bao la Mkhitaryan alilifunga akiwa ameotea ‘offside’ na Olivier Giroud alifunga akiwa ‘onside’, hakuwa ameotea.

Mchambuzi wa Sky sports na mchezaji wa zamani wa Manchester United, Gary Neville, amekaririwa akisema kuwa bao la Giroud ni bora zaidi kuwahi kuliona tangu aanze kufuatilia soka.

Kwa Giroud mwenyewe licha ya kupokea sifa hizo alikiri kuwa alikuwa na bahati kufunga bao hilo na hakuwa amepanga kufanya kilichoonekana.

“Kwanza Alexis alinipa pasi ya nyuma, nilijaribu kupiga kwa kisigino na kwa bahati nzuri malengo yangu yakaenda sawa,” alisema Giroud alipohojiwa na kituo cha Sky Sports.

“Sikuwa nimesimama vizuri japo nilikuwa na mawazo ya kufunga kwa namna ile tangu krosi ya kwanza niliyopewa na Nacho, ni jambo jema kwa timu kwa kuwa nimefunga na tumepata pointi muhimu.”

Mchambuzi mwingine wa Sky Sports, Graeme Souness, alimpongeza Giroud kwa namna alivyokuwa na uharaka wa kuunganisha krosi ile japo alikiri pia bahati ilimbeba straika huyo.

“Bao la kisasa sana alilofunga Olivier Giroud,” alisema Souness.

“Ni bao bora sana lakini nafikiri mchezaji mwenyewe ndiye anayeweza kutoka hadharani na kusema kuwa alibahatisha kwenye upigaji ule.

“Nina uhakika hata akipewa mipira mingine 1,000 kama ile hawezi kupiga na kufunga. Alikuwa na bahati kwa wakati ule kupiga na kufunga.

“Kama mpira ule usingekwenda nyavuni nina hakika angerudi na kumwambia Sanchez kuwa angeupiga ule mpira kwa mbele ili apige kichwa.”

Naye Jamie Redknapp alisema: “Ni bao bora, siwezi kuliweka kwenye chungu kimoja na bao la Thierry Henry alilowafunga Manchester United kipindi kile, au ile ‘tik-tak’ ya Wayne Rooney dhidi ya Manchester City, hili ni bao bora unaloweza kulitazama kwa wakati mmoja na lile alilofunga Mkhitaryan.”

Kwa upande wa Jamie Carragher, yeye alisema: “Ni maajabu kwakweli. Unaweza kuduwaa kwa muda ukilitazama lile bao. Ni aina ya mabao ambayo utachukua muda kidogo kuyaamini.

“Alidhamiria kufunga, siamini kama kulikuwa na chembe ya bahati katika lile. Muhimu alionekana alikuwa na dhamira ya kupiga basi huwezi kusema kuwa alibahatisha.”

Lakini pamoja na mjadala huo, wataalamu hawa walikubaliana nini katika swali lile la lipi bao bora katika haya mawili?

Kwa mujibu wa Carragher, kura yake ilienda kwa Giroud akisifu namna Arsenal walivyoshirikiana kwa pamoja katika kulitengeneza bao hilo.

“Nafikiri kabla hatujakaa na kumpongeza Giroud ni lazima turudi nyuma na kuisifia Arsenal kwa namna walivyoshirikiana kutengeneza bao hilo,” alisema Carragher.

“Kwa upande wangu bao la Giroud ni bora kwa namna shambulizi lilivyotengenezwa kutoka mwanzo mpaka mwisho.

“Awali wote tulikuwa upande wa Mkhitaryan kuwa alifunga bao la msimu, licha ya kuwa alilifunga akiwa ‘offside’ lakini sasa ni lazima wote tukubaliane kuwa Giroud amefunga bao bora zaidi.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -