Saturday, November 28, 2020

NANI AMEMTUMA PETER MHINZI KUWANIA DRFA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

MCHAKATO wa Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), unaendelea ambapo umepangwa kufanyika Aprili 9 mwaka huu.

Mwonekano wa uchaguzi wa chama hicho ndio utakaotoa picha halisi kuelekea mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Kwa kuwa Dar es Salaam ni makao makuu ya TFF, utaona kwamba uchaguzi wa DRFA unakuwa na fitina nyingi tofauti za zile zinazofanyika katika vyama vya soka vya mikoa mingine.

Mchakato wa uchukuaji na urejeshwaji wa fomu ulitarajiwa kufungwa jana jioni, lakini hadi kufikia Jumamosi iliyopita watu 20 walikuwa wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho.

Watu waliochukua fomu ni pamoja na mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA), Peter Mhinzi.

Mhinzi anawania nafasi ya mwenyekiti wa DRFA ambaye mwaka uliopita alipata msukosuko kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura, baada ya kuingia mkataba kinyemela na mfanyabiashara mmoja.

Ilikuwa ni ziara ya kushtukiza ya Naibu Waziri  huyo aliyetembelea ofisi za (TEFA) na kukutana na madudu ya Mhinzi.

Kilichomshangaza Naibu Waziri huyo ni kukuta uwanja wa soka wa Tandika Mabatini kutumika katika shughuli za kuchomea vyuma.

Kitendo hicho kilimwacha mdomo wazi Naibu Waziri Annastazia na alipohoji kulikoni uwanja wa soka umebadilishwa matumizi ya soka, alipatwa na butwaa alipojibiwa.

Mfanyabiashara aliyekuwa akifanya kazi za kuchomea vyuma katika uwanja huo, alimjibu Naibu Waziri Annastazia kuwa aliingia mkataba na TEFA ambayo ipo chini ya Mhinzi ili waweze kufanyia shughuli zake hapo.

Lakini kitu kilichomshangaza zaidi Naibu Waziri Annastazia aliposikia kwamba mkataba wa mfanyabiashara huyu ulikuwa ni siri ya Mhinzi na viongozi wenzake, huku klabu wanachama wa TEFA wakiwa hawajui lolote lililokuwa likiendelea mpaka ilipokuja kujulikana katika ziara ya Naibu Waziri.

Kutokana na sababu hizo, Uwanja wa Bandari ulikuwa unatumika kwa mashindano mbalimbali yaliyokuwa yakiandaliwa na TEFA baada ya ule wa TEFA kuuzwa kinyemela.

Leo hii kama Naibu Waziri Annastazia asingechukua hatua ya kumfukuza mfanyabiashara huyu, klabu wanachama wa TEFA wangeendelea kuteseka kutokana na uwanja wao kugeuzwa kuwa  dili kwa Mhinzi na wenzake.

Klabu wanachama wa TEFA wataendelea kumshukuru na kumkumbuka Naibu Waziri Annastazia aliyeweza kuurejesha uwanja wa soka wa Tandika mikononi mwao na leo unaendelea kutumika katika michezo ya soka.

Ukiondoa hilo, utaona kwamba soka la Temeke kwa sasa linaonekana wazi limekufa baada ya Mhinzi na wenzake kuingia madarakani.

Kabla ya Mhinzi kuingia madarakani kulikuwa na zaidi ya timu 100 zilizokuwa zikicheza soka wilayani Temeke, lakini kwa sasa hazifiki idadi hiyo.

Kwa sasa Temeke hakuna hata timu moja inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, baada ya Tesema kupigwa bei na viongozi hao wa Tefa  iliyonunuliwa na Manispaa ya Kinondoni.

Timu hiyo kwa sasa inaitwa KMC inashiriki Ligi Daraja la Kwanza, lakini Mhinzi aliiuza timu ya Mapambano iliyokuwa imepiga hatua kwa kufikia kushiriki Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Huyu ndiye Mhinzi ninayemjua, anayetaka kwenda kuwa mwenyekiti wa DRFA akiwa ana madudu mengi katika chama chake anachokiongoza cha TEFA.

Anakwenda kuwania uenyekiti wa DRFA ametumwa na nani? Aliyemtuma anajua TEFA wanakusanya zaidi ya Sh milioni tatu kwa mwezi na wanalipa kodi ya Serikali?

Lakini Mhinzi analipa ipasavyo kodi ya ardhi kutokana na kumiliki Uwanja wa Tandika Mabatini kwa mujibu wa taratibu za Serikali?

Ni kitu gani anachofuata DRFA kama ameshindwa kuongoza TEFA kwa maana ya kushindwa kupandisha timu Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Kuu Bara kwa miaka zaidi ya tisa aliyokaa madarakani.

Wadau wa soka Mkoa wa Dar es Salaam wanatakiwa kumpima Mhinzi kwa madudu anayoyafanya Temeke kabla hawajafanya kosa la kumchagua, ambalo watajutia kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

kapssmo@gmail.com 0716985381

Tukutane Jumatatu ijayo

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -