Friday, October 23, 2020

NANI AMEMWOMBA MSAMAHA SAMATTA KUIKOSA AFCON 2017?

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

KUOMBA msamaha si jambo zito kwa binadamu yeyote mstaarabu na anayejielewa. Watanzania wengi tumekuwa tukisifika kwa utamaduni huo.

Hata hivyo, huenda tumejisahau kidogo kwa kile tulichomfanyia nyota wetu, Mbwana Samatta. Tunapaswa kumpigia magoti kwa kushindwa kumwezesha kucheza fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (Afcon 2017) zinazoendelea nchini Gabon.

Kwa kile ambacho ameshakifanya, alistahili kuwa nchini humo na kama mafanikio binafsi ya mchezaji yangekuwa yakimwezesha kuingia Afcon 2017, basi leo hii tungekuwa tukimtazama Samatta pale Gabon.

Kwa juhudi ambazo amezifanya tangu alipoondoka Simba ambayo ndiyo iliyomuweka kwenye ramani ya soka, alikuwa na nafasi yake kwenye michuano hiyo.

Ukiachana na klabu anayoichezea sasa ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, mafanikio yake akiwa na TP Mazembe ikiwamo kuiwezesha kunyakua taji la Klabu Bingwa Afrika, yalitosha kumpeleka Gabon mwaka huu.

Lakini pia, miaka miwili iliyopita, aliiweka Tanzania kwenye ramani ya soka kwa kushinda tuzo ya Mchezaji Bora Afrika wa Ligi za Ndani.

Ndiye Mtanzania pekee anayecheza ligi kubwa barani Ulaya kwa sasa. Kwanini juhudi zote hizo zimemnyima nafasi ya kuonekana ‘duniani’ kupitia Afcon 2017?

Lazima viongozi, wachezaji na wadau wa soka hapa nchini wakubali kuwa Samatta amefanya kazi kubwa kuliko wao na hiyo ndiyo sababu anastahili kuombwa radhi.

Kwa maana nyingine, huenda Tanzania haikustahili kucheza Afcon 2017 lakini nafasi ya Samatta kwenye michuano hiyo ilikuwepo. Kwanini tuendelee kuwa wanafiki kwa kushindwa kukiri kuwa katika soka la hapa nchini, Samatta amefanya juhudi kubwa kuliko Watanzania wote?

Tangu mwaka 1980, kipindi ambacho Tanzania ilicheza Afcon kwa mara ya mwsiho, ni kiongozi gani ametupeleka katika fainali hizo japo tukaishia hatua ya makundi kama majirani zetu Uganda walivyofanya mwaka huu?

Baada ya kumalizika kwa fainali hizo zilizofanyika jijini Lagos, Nigeria, ni ubabaishaji tu umekuwa ukiendelea katika uongozi wa soka hapa nchini.

Mfano; katika kipindi kifupi kisichozidi miaka 20, Samatta amecheza Mbagala Market, akaenda Simba, akatimkia Mazembe na sasa yuko Genk ya Ubelgiji.

Tukija kwa viongozi wa soka letu, ni mkakati gani wa maendeleo ya soka ulioanzishwa miaka 15 iliyopita, ambao kwa sasa Tanzania inanufaika nao? Hakuna.

Hebu tujiulize, kwa kipindi hicho, ni wachezaji wangapi wa Tanzania wameweza kujenga ufalme wao katika klabu zenye hadhi kubwa barani Afrika kama alivyofanya Samatta akiwa na Mazembe?

Kwanini tusiamini kuwa tulikuwa ‘wachawi’ wa Samatta kwenye mipango yake ya kucheza Afcon 2017? Binafsi naamini hivyo. Ukweli ni kwamba tumeshindwa kuendana na kiu yake ya mafanikio.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -