Saturday, November 28, 2020

NANI ATANISHAWISHI KWA HILI LINALOENDELEA LIVERPOOL?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

JUMATATU ile, ya usiku ule. Pale pale ambapo Jamie Vardy alijikunja na kuunyoosha mguu wake wa kulia akimtungua Simon Mignolet, aliirudia tena historia. Liverpool ikafa bao 3-1 dhidi ya mabingwa watetezi waliochoka, Leicester City.

Je, walitaka kutuaminisha wadau wa soka kwamba lengo lao la ‘top four’ halitatimia mwaka huu kama Jurgen Klopp anavyokumbushia kila siku? Mashaka yalitawala na jamii nzima ya wanazi wa Liverpool walizidi kuchanganyikiwa.

Kile kipigo cha Leicester kilikuwa ni mwendelezo tu wa Liverpool yenye nguvu na mamlaka dhidi ya hizi timu zilizo na hadhi ya kuitwa ‘timu kubwa’, lakini isiyoweza kuonesha makucha yake dhidi ya timu za kiwango cha kati ambazo wengine huziita timu ndogo.

Na ndio maana sikushangazwa kuyaona mabao matatu yaliyotinga kwenye nyavu za Petr Cech, usiku wa juzi pale Anfield ulikuwa na asilimia nyingi za kuiona Liverpool ikishinda mbele ya mwanafunzi mwenzake wa darasa moja la ubora, timu ambazo zina hadhi ya kumaliza ndani ya nafasi tano za juu.

Nilipoitazama Liverpool iliyocheza King Power na hii ya juzi pale Anfield, akili yangu iligoma kukubali kwamba Liver ilikuwa haimtaki Zlatan Ibrahimovic.

Baada ya Jamie Vardy kufungua akaunti ya mabao kwa timu iliyokuwa chini ya kocha wa muda, Craig Shakespare, ni mchezaji gani wa Liverpool ambaye alikuwa tayari kujitwisha mzigo mzito? Sikumwona yeyote. Na kutokuwepo kwake ndiko kulipelekea Leicester kufurahia soka lao na kufunga walivyotaka.

Liverpool walikuwa na asilimia nyingi za kumbamiza Arsenal wakiwa na Coutinho, Firmino na Mane. Si kitu kigumu sana hicho kwao, lakini watakuwa na shughuli nyepesi mno wikiendi hii dhidi ya Burnley kama safu yao ya ushambuliaji ingekuwa na mchezaji wa kariba ya Zlatan.

Ukiniuliza ni nafasi gani yenye ubora zaidi pale United, inayoibeba klabu ni pale kwa Ibracadabra. Mabao yake zaidi ya 20 ni muhimu mno kwa timu yenye njaa na makombe. Mataji mawili yaliyoongezeka kwenye kabati la makombe pale Old Trafford, yote yamechangiwa kwa asilimia kubwa na Zlatan.

Paul Pogba? Henrikh Mkhitaryan? Hawa ni wachezaji wazuri kwa nafasi na majukumu yao, lakini ni Ibrahimovic.

Kwanza ni mzoefu, anatambua kila njia ya kusaka mafanikio yake na klabu. Hatingishwi na kila aina ya presha. Liverpool inamkosa mchezaji wa namna hii, kama alivyokuwa Luis Suarez mwaka 2014, Muuruguay ambaye aliifanya timu nzima ionekane bora kwa jinsi alivyojitoa uwanjani. Alikuwa mchezaji wa mfano.

Ni kwa namna gani Liverpool itaweza kuwa na mtu wa aina hii? Kutumia fedha kama mahasimu wao. Si falsafa ya Klopp, lakini upepo wa sasa utamlazimu atumie fedha kukiongezea nguvu kikosi chake kwenye maeneo yenye mapengo sugu.

Klopp anasisitiza kila uchwao kwamba mipango yake ni ya muda mrefu, kikosi alichonacho ndio mpango wenyewe, lakini ni mpango unaoathiriwa na kiwango kisichokuwa na msimamo mechi baada ya mechi.

Usikiapo lawama za mashabiki, tambua kuwa wamechoshwa na mbinu zake. Mbinu nzuri zisizoonekana kwa macho ya kawaida. Klopp amekuwa ni nabii wa kile anachokiamini, lakini imekuwa ngumu kwake kukubalika na wote.

Kwa sasa Klopp hawezi kufanya miujiza yoyote, kwa msimu huu hatakuwa na muda wa kutosha wa kufanya hivyo. Wa kumuokoa na matokeo yasiyokuwa na mwendelezo mzuri alikuwa ni Ibrahimovic wake mwenyewe. Je, atagoma kuwa naye msimu ujao na kuendelea kuamini misimamo yake?

Nani anaweza kunishawishi kwamba Liverpool itaendelea kuwa kituko cha kupora wenye nacho na kugawa kwa wasio nacho?

Nasubiri kuona Klopp akitimiza kile alichokiahidi. Kusajili na kuliongezea nguvu jeshi lake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -