Wednesday, November 25, 2020

Nani atapotea ndani ya kizazi hiki cha dhahabu?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

JARIDA maarufu la soka na lenye heshima duniani la World Soccer liliwahi kuwaorodhesha wachezaji makinda wenye kiwango cha hali ya juu mwaka 2007, ambapo baadhi ya waliokuwepo walikuwa Juan Mata, Mesut Ozil, Karim Benzema, Ivan Rakitic, Sergio Aguero na Gareth Bale, ambao walifanikiwa kunyakua mamilioni, kushinda tuzo kubwa michezoni pamoja na kujizolea umaarufu duniani kote.

Makinda wengine wa wakati huo, Giovani Dos Santos, Bojan Krkic na Gregory Van Der Wiel ambao waliwavutia wengi kutokana na viwango vyao vya soka, lakini hawakuweza kudumu kwa muda mrefu.

Pia vijana kama Sadick Adams, Dumitru Copil, Gerardo Bruna, Andrea Russotto, Nour Hadhria nao walipata umaarufu mwaka huo, lakini walipotea baada ya miezi michache.

Beki chipukizi wakati huo, Breno Borges, ambaye alisifiwa kwa uwezo wake wa kusakata soka, akifananishwa na gwiji wa zamani wa Ujerumani, Franz Beckenbauer, aliishia gerezani baada ya kufanya jaribio la kutaka kuichoma nyumba yake.

Hakuna kilichobadilika sana kwa muongo mmoja uliopita. Hivi sasa kufanya utabiri juu ya chipukizi hawa imekuwa ni jambo gumu, lakini kwa miaka mitatu ya hivi karibuni, 2014, 2015 na 2016 kumejitokeza makundi ya wachezaji wadogo wenye ubora zaidi katika klabu za ligi kuu pamoja na akademi zote duniani.

Wachezaji waliotabiriwa makubwa kuanzia mwaka 2014, tayari wamepiga hatua kubwa hivi sasa, Marcus Rashford amenyakua taji la FA, ameifungia timu yake ya taifa ya England na ameshaanza kuimiliki nafasi ya nahodha wake kwenye klabu ya Manchester United (Wayne Rooney).

Ousmane Dembele tayari amepata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa na msimu huu anaichezea klabu ya Borussia Dortmund, iliyomsajili kwa pauni milioni 15.

Lakini makinda wengine bado wanaendelea kukua kisoka na waliobaki pia wanaweza kushindwa kufikia kile tulichokitabiri kwao.

Kadiri muda utakavyosonga mbele tutajua ni umbali gani ambao vijana hawa watafika, lakini wewe unadhani ni mchezaji gani atakayeweza kufika mbali zaidi ndani ya orodha hii ya makinda hawa kulingana na viwango vyao ndani ya timu zao?

MAKINDA 10 BORA DUNIANI

Marco Grujic (Liverpool)

Gianluigi Donnarumma (AC Milan)

Marcus Rashford (Manchester United)

Alex Iwobi (Arsenal)

Renato Sanches (Bayern Munich)

Viktor Kovalenko (Shaktar Donetsk)

Delle Alli (Tottenham)

Moussa Dembele (Celtic)

Marco Asensio (Real Madrid)

Aleksandr Golovin (CSKA Moscow)

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -