Tuesday, October 20, 2020

NANI HAJAWAHI KUWA MNAFIKI KWA NGASSA, LUIZIO?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HASSAN DAUDI

UNAFIKI umekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku. Tumekuwa tukiishi hivyo kwa miaka mingi na umekuwa utamaduni wetu. Kama tabia hiyo ingekuwa nguo, basi ningependekeza liwe vazi la taifa.

Utakapoulizwa na rafiki yako juu ya mchumba wake anayetarajia kumuoa, utammwagia sifa kibao huku moyo wako ukikusuta kuwa unachokizungumza hakina ukweli wowote.

Baadaye utakaa na watu wengine na kuanza kumponda mshikaji wako ukisema msichana anayetaka kumuoa ni mbaya. Hatuko tayari kusema ukweli hasa pale tunapohisi kuwakera wale tunaowaheshimu. Huo ndiyo unafiki wenyewe.

Nilikuwa mmoja wa waliokuwa wakifuatilia kwa ukaribu harakati za dirisha dogo la usajili lililofungwa siku chache zilizopita.

Yapo mengi niliyoyashuhudia kwa kipindi chote hicho, lakini kitendo cha mastaa Mrisho Ngassa na Juma Luizio kurejea Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL), kilinishitua kidogo.

Ngassa maarufu kwa jina la ‘Uncle’ alisaini kuichezea Mbeya City huku Luizio akijiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Nyota hao wote walikuwa nje ya nchi wakisakata soka la kulipwa, hivyo kurudi kwao hapa nchini halikuwa jambo la kawaida.

Kama nilivyosema hapo awali, unafiki umekuwa mfumo rasmi wa maisha tunayoishi. Huenda watu wao wa karibu wakabaki wakiwasifia na kushindwa kuwauliza maswali ya msingi.

Kama si unafiki wetu, watu wa karibu wa mastaa hao walipaswa kuwaambia wamekuja kumalizia maisha yao ya soka.

Ni rafiki gani wa Ngassa anayeweza kumwambia nyota huyo amekuja kujiandaa kustaafu? Kwani marafiki zake hawajui kama hicho ndicho kilichobaki kwa mshikaji wao? Naomba niwe wa kwanza kuukataa unafiki huo.

Ukiiangalia safari ya Ngassa mpaka alipojiunga na Mbeya City hivi karibuni, huwezi kumfikiria Ngassa kwenye orodha ya Watanzania 10 watakaocheza Ulaya baadaye.

Ni wazi winga huyo wa zamani wa Kagera Sugar amekuja kumalizia kipindi kifupi kilichobaki kwenye maisha yake ya soka. Naamini ninachokitabiri kimo pia kwenye kichwa cha Ngassa.

Baada ya kuondoka Yanga, Ngassa alitua Ligi Kuu Afrika Kusini ambako alikuwa akikipiga katika klabu ya Free State.

Huko, mambo hayakwenda vizuri kwani michezo mingi ya kikosi hicho aliishuhudia akiwa benchi.

Aliamua kufungasha virago vyake na kutua Oman alikosajiliwa na mabingwa wa nchi hiyo, Fanja FC.

Kwa mawazo yangu yasiyo ya kiweledi, niliamini Ngassa amejifunza kitu. Nilitegemea kumuona akizaliwa upya pale Sudan.

Nilitamani kuona akiwaumbua mabosi wake wa Fre States akiwaonyesha kuwa walibugi kumwacha aondoke ‘Sauzi’.

Kinyume na mawazo yangu, hakukuwa na mabadiliko yoyote na kilichofuata ndicho hicho tulichokishuhudia siku chache zilizopita, kujiunga na Mbeya City.

Kwa safari hiyo, nini kinachotuzuia kumwambia amemaliza safari ya kwenda kukipiga barani Ulaya?

Nikiweka kando unafiki ambao umekuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya Watanzania, nataka kuwa wa kwanza kuamini kuwa nyota huyo hawezi kufika kule aliko Mbwana Samatta.

Najua wapo wanaoweza kukaa na Ngassa na kumwambia kuwa bado ana safari ndefu kwenye soka. Sitaki kuwa miongoni mwa wanafiki hao.

Labda anaweza kutuachia kumbukumbu nzuri ya kufunga mabao ya ‘kideo’ akiwa na Mbeya City lakini si kufika kule ambako hata yeye angetamani kuwa, yaani kuicheza soka barani Ulaya.

Kwa upande wa Luizio, sikutaka kuamini kuwa beki huyo wa zamani wa Mtibwa angekubali kuachana na Zesco ya Zambia na kurudi Bongo.

Simaanishi kuwa alitakiwa kung’ang’ania kukaa benchi pale Zesco, la hasha. Lakini, alipaswa kufikiria mara mbili kabla ya kuamua kurudi nyumbani.

Nani anayempenda Luizio kiasi kwamba anaweza kumwambia uamuzi wa busara ulikuwa ni kuangalia ni jinsi gani atapiga hatua kwenda mbele alipofeli Zesco?

Hakuna anayeweza kumwambia hivyo, ila wapo wengi wanaoweza kukaa mbali naye na kuwaambia watu kuwa alikuwa mjinga kukubali kucheza tena ‘ligi ya madafu’.  Unafiki umeshayateka maisha yetu bwana.

Bila shaka kabla ya kusajiliwa na Mtibwa, ndoto yake kubwa ilikuwa ni kukipiga VPL. Baada ya kujiunga na mabingwa hao wa soka mjini Morogoro, alitamani kupata nafasi ya kutoka nje ya nchi.

Kuichezea Zesco ilikuwa ni hatua moja ya kusonga mbele lakini ameamua kurudi nyuma na kutua Bongo. Nani amemwambia hivyo? Naamini hata watu wake wa karibu wanamficha kuwa miaka miwili au mitatu ijayo atasajiliwa na timu ndogo. Ni unafiki kila hatua ya maisha yetu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -