Tuesday, November 24, 2020

NANI WA KUMZUIA CHELSEA?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...
  • akishinda mechi tano tu anachukua mwari wake

    KAMA kuna waliodhania ushindi wa Tottenham wa mabao 4-0 dhidi ya Watford, ambao ulipunguza pengo la pointi kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwa nne, ungeweza kuwaathiri vinara wa ligi hiyo Chelsea. Kocha wa Blues, Antonio Conte,  amewaonyesha kwamba hakwenda England kushangaa nyumba za kimalkia, kuichapa Bournemouth 3-1 na kulifanya pengo hilo la pointi na kuwa saba kama mwanzo.

Spurs walitangulia kucheza mechi yao Jumamosi mchana kisha Blues walishuka dimbani usiku na sasa watakuwa wakisaka ushindi katika mechi tano kati ya saba zilizobakia za ligi hiyo ya England.

Bao la kujifunga la Adam Smith na mabao mengine kutoka kwa Eden Hazard na Marcos Alonso yaliifanya Chelsea kukusanya pointi 75 katika michezo 31 na kuwaacha tena Spurs kwa pointi saba na sasa wanawinda pointi hizo 15.

Kutokana na mechi ambazo Chelsea wamebakiza katika ratiba yao, je ,ni nani ataweza kuwazui wasishinde mechi tano na kukusanya pointi 15 na kubeba ubingwa?

 

 

Man Utd (ugenini) –

Jumapili hii (Aprili 16)   

Kwenye vyombo vya habari mechi ngumu iliyobaki dhidi ya Chelsea ni safari yao ya Old Trafford. Klabu hiyo ya London imefanikiwa kushinda mechi tatu ndani ya miaka 12 katika mechi walizocheza nyumbani kwa Manchester United na kikosi hicho cha Jose Mourinho kimekuwa kwenye wakati mgumu kwenye uwanja wao wa nyumbani.

United wako kwenye hatari ya kuweka rekodi ya kukusanya mechi chache kwenye uwanja wa nyumbani katika historia ya Ligi Kuu Englandare na Chelsea wataenda wakijiamini baada ya kuichapa mabao 4-0, katika mechi ya kwanza na kurudia tena kichapo cha 1-0 kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA katika Dimba la Stamford Bridge.

 

 

 

Southampton (nyumbani) – Jumanne, Aprili 25, 2017

Baadaye mwezi huu, Chelsea watakuwa na kibarua kingine cha kuvaana na Southampton, wakati kikosi cha Claude Puel kikiwafuata kwenye Dimba la Stamford Bridge siku tatu baada ya Blues kucheza mechi yao ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham. Conte atahakikisha kikosi chake kinajiweka sawa na kuwa tayari bila kujali kama watakuwa wamefuzu fainali ya FA. Lakini wakati huo watakuwa wameangalia ushindi wa timu nyingine na kuchukua kama changamoto kabla ya kuvaana na Southmpton.

 

 

Everton (ugenini) –

J’pili, Aprili 30, 2017

Uwanja wa Goodison Park si wa mchezo mchezo na kocha wa Everton, Ronald Koeman, anaweza kusababisha majanga kwa Blues kutokana na kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ikiongozwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Romelu Lukaku ambaye kwa sasa anaongoza kwa mabao Ligi Kuu England. Lakini Chelsea waliichapa Everton mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Novemba mwaka jana na watakuwa na uhakika wa kumaliza mwezi huu wakiendelea kuwa kileleni.

 

 

Middlesbrough (ugenini)

– Jumatatu, 8 Mei, 2017

Huenda Middlesbrough wakaendelea kuwa kwenye hatari ya kushuka daraja na kurejea ‘Championship’ watakapokuwa wageni wa Chelsea, Mei 8, mwaka huu. Lakini kikosi hicho cha Conte kilifanikiwa kushinda bao 1-0 pekee kwenye Uwanja wa Riverside, Novemba mwaka jana na inaweza ikawa mechi nyingine ngumu kwao watakapokutana tena. Baada ya Boro kuichapa Hull City Jumatano ya wiki iliyopita, sare yao 0-0 dhidi ya Swansea na Burnley pamoja na matokeo mengine, ni ishara kwamba wana uwezo wa kumbana mpinzani yeyote mbele yao.

 

 

West Brom (ugenini) –

J’mosi, Mei  13, 2017

West Brom walivuruga matumaini ya Tottenham kwa kutoka sare White Hart Lane Aprili mwaka jana, pia wanaweza kufanya hivyo msimu huu. Chelsea wataenda kwenye uwanja huo Hawthorns wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 3-0 Desemba mwaka juzi, msimu ambao walibeba taji.

 

 

Watford (ilihairisha)

Chelsea na Watford wanasubiri siku ya kupangiwa kucheza mechi hiyo, huku wakiwa wametoka kuchapwa mabao 4-0 dhidi Spurs juzi, Chelsea wana uhakika wa kuchukua pointi kutoka katika mechi hii, lakini walibanwa hadi dakika 10 za mwisho kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa Agosti mwaka jana. Msimu huu Watford wamefanikiwa kuifunga Man United na Arsenal na wanaweza kuwavurugia Blues mipango yao.

 

 

Sunderland (nyumbani)

 – Jumapili, Mei 21, 2017

Chelsea watakuwa na kazi rahisi ya kumaliza mechi yao ya mwisho Stamford Bridge dhidi ya Sunderland, kikosi ambacho kwa sasa kinashika mkia katika msimamo wa Ligi Kuu England. Blues waliichapa Sunderland 3-1 kwenye mechi ya mwisho ya msimu wa 2014/15, ambao walibeba taji na wanaweza kurudia hilo msimu huu, ingawa msimu huu waliifunga Sunderland 1-0 kwa tabu Desemba mwaka jana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -