Thursday, November 26, 2020

NAPE AKINUKISHA PEUPEE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ametema cheche katika mkutano wake na waandishi wa habari alioufanya nje ya Hoteli ya Protea, baada ya kuzuiwa kufanyia ndani.

Nape alipanga kufanya mkutano huo baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa kipindi cha mwaka mmoja, ambapo kwa sasa mrithi wake atakuwa ni Harrison Mwakyembe, katika mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli.

Katika mkutano huo alipongeza uamuzi wa Magufuli kwa kuweza kumwamini kama kijana na kumpa heshima ya kuingia kwenye Baraza la Mawaziri moja kwa moja, akiomba watu kumuunga mkono aliyeziba nafasi yake, Mwakyembe.

“Nampongeza Rais wangu Magufuli kwa maamuzi aliyofanya, aliniamini kwa mwaka mmoja kama kijana wake, akanipa heshima ya kuingia kwenye Baraza moja kwa moja, namshukuru sana na kama alivyoniamini, ndivyo anadhani ameona imetosha na anamweka kaka yangu Mwakyembe, namuunga mkono, nampongeza kwa kuteuliwa, yeye ni mwanahabari na mwanasheria, naamini atasimamia haki,” alisema.

Wakati Nape akiyasema hayo, wadau mbalimbali kwenye sekta mbalimbali za michezo na burudani kila mmoja alitoa maoni yake kufuatia mabadiliko hayo, ambayo yanaanza mara moja baada ya kuapishwa hapo leo.

Katibu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani Namkoveka, alishindwa kuzungumza chochote mara baada ya kuomba muda kutokana na mshutuko alioupata baada ya taarifa hiyo ya kuondolewa kwa Nape.

“Hivi ni kweli unayoniambia, mbona sifahamu hizo taarifa? Kwa sasa siwezi kuzungumza chochote, labda kesho (leo), kwani naongoza watu wengi hivyo siwezi nikakurupuka kutoa chochote kwa sasa mpaka nitakapokuwa nimefikiri vya kutosha,” alisema Namkoveka.

Kwa upande wa Katibu wa Chama cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST), Antony Ruta, alisema wamepokea vema mabadiliko hayo, lakini Nape aliweza kuongoza vizuri katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani.

“Tunampokea Mwakyembe, kwani najua ataweza kutusaidia upande wa sheria, kwa kuwa ngumi mara nyingi zimekuwa zikikumbwa na migogoro. Lakini hiyo haitufanyi kusahau yale yote aliyofanya Nape kipindi cha uwaziri wake.”

Nao wasanii mbalimbali walimzungumzia waziri huyo wa zamani, Nape ambapo rapa Abbott Charles ‘Quick Rocka’, alisema: “Sifurahii kuwa Mtanzania tena, tunatangazaje na kuisifia nchi ambayo viongozi wanaosimamia ukweli na sheria wanaondolewa, Nape alikuwa waziri sahihi kabisa kwetu wasanii, wanamichezo na wanahabari.”

Msanii wa Bongo Movies, ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake nchini Denmark, Issa Mussa ‘Cloud 112’ na yeye alisema: “Huyu ndiye shujaa na mwokozi wa kazi zetu za sanaa. Sasa giza nene limetanda.”

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Zainabu Mbiro, alisema chama chao kipo tayari kufanya kazi na yeyote yule, kwani wanachoangalia ni kusonga mbele kwenye netiboli, si vinginevyo.

“Sijafurahi wala sijakasirika, netiboli ipo pale pale, hata akija nani, ndiyo maana tupo tayari kufanya kazi na yeyote yule atakayeteuliwa na rais wetu. Kwa kuwa sisi tunafanya kazi na Wizara ya Michezo,” alisema.

Wakati Chaneta kikitoa tamko hilo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rais wake, Jamal Malinzi, wamempongeza Dk Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

“Tunaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania tutapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya michezo, Mungu amwongoze katika kutekeleza majukumu yake,” alisema Malinzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -