Wednesday, October 28, 2020

NAPE AWAONGOZA MAMIA KUMUAGA AMINA ATHUMANI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA JESSCA NANGAWE


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, jana aliwaongoza mamia ya waombolezaji katika tukio la kuuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari za michezo na burudani wa Kampuni ya Uhuru Publishers, Amina Athuman,  aliyefariki juzi kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya uzazi.

Kabla ya kuanza kuugua na hatimaye kufariki dunia, marehemu Amina alikuwa miongoni mwa waandishi wa habari waliokuwa wakiripoti michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyofikia tamati mjini Unguja Januari 13 kwa timu ya Azam FC kutwaa ubingwa.

Akizungumza wakati wa tukio la kuagwa mwili wa marehemu Amina, Waziri Nnauye, alisema tasnia ya michezo imempoteza mmoja wa waandishi wachapakazi na aliyekuwa akifanya kazi zake kwa umakini mkubwa, huku akiitaka familia yake kuwa na moyo wa subira kufuatia kifo hicho.

“Alikua ni moja ya waandishi wenye kujituma sana katika kazi yake, tulifahamu uwezo wake, kikubwa ni kumwombea makazi mema huko alipo, yeye ametangulia na sisi tupo nyuma yake, tunawapa pole wanafamilia kutokana na msiba huu mzito,” alisema Nape.

Mwili wa marehemu Amina ulitarajiwa kusafirishwa jana kuelekea Lushoto Tanga, huku shughuli za maziko zikipangwa kufanyika leo.

Roho ya marehemu Amina ipumzike mahali pema peponi, amina.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -