Wednesday, November 25, 2020

NASHANGAZWA KUONA WIJNALDUM ANAJARIBIWA LIVERPOOL

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

Na Kelvin Lyamuya

USIKU wa Jumamosi kuamkia jana Jumapili kulikuwa na sherehe za mashabiki wa Liverpool, ni kama ulikuwa mchezo wa mwisho wa ligi na ubingwa ulitua Anfield. Hatari.

Kelele hazikuwa kwa sababu ya ubingwa, lakini ile ilikuwa ni furaha ya kuwa juu ya mahasimu wao wakubwa, Manchester United. Ni kama mashabiki wa Spurs wanavyoshangilia kila mwisho wa msimu wanapomaliza juu ya Arsenal, ndio kawaida yao kule.

Liverpool ilipata ushindi wake wa kwanza mwaka huu na wamefanikiwa kuonja ushindi wa kwanza wa ligi. Ni aibu eti? Hiyo ndio Liverpool mliyodhani itachukua ubingwa, ikaporomoka kutoka nafasi ya pili. Ikaondolewa kwenye makombe mawili, ikaondolewa kwenye mbio za ubingwa wa ligi.

Lakini ushindi dhidi ya Spurs bado unawapa nguvu ya kumaliza nafasi nne za juu. Ushindi mtamu, lakini usingeweza kuwa mtamu zaidi kama Sadio Mane asingekuwapo. Na utamu usingekolea zaidi iwapo Giorginio Wijnaldum asingecheza.

Wijnaldum ni ‘TANK’ (gari maalumu la kivita litumikalo jeshini, kubwa mno). Lakini jamaa si mkubwa kiumbo, ila kwa jinsi achezavyo, mtanisamehe, nitaendelea kumwita hivyo.

Wanachoshindwa kuelewa watu ni kuwa Liver haina wachezaji wenye moyo wa kupigania mataji, uzoefu wengi hawana. Wengi wametoka kwenye timu za kawaida. Hata huyu Wijnaldum katoka huko huko lakini kwa alichonacho akilini mwake ni cha ziada, si mtu wa kujaribiwa.

Pale Liver aliyewahi kuonja raha na kujua jinsi ya kupambana kwa ajili ya taji ni Milner, si Lallana, Henderson wala Mane! Lakini naiona roho ya upambani kwa Wijnaldum.

Liver wana bahati kuwa naye, ni mchezaji wa mipango ya muda mrefu.

Dhidi ya Spurs alifanya vitu muhimu vilivyozalisha matokeo kwa Liver. Wakati Mane anafunga, Wijnaldum alikuwa mashine muhimu kutoka nyuma.

Uliwaona Mousa Dembele na Victor Wanyama? Achana na Christian Eriksen ambaye alitolewa mapema kipindi cha pili. Hii safu ya kiungo ya Spurs ilipotezwa vibaya na Wijnaldum.

Jamaa wako vizuri mno, wanajua kutumia nguvu yao kwa nidhamu ya hali ya juu, wana kadi chache za njano lakini ukweli ndio huo, huwezi kufanya lolote mbele yao kama huna roho ya upambanaji.

Katika mchezo uliokuwa ‘open’ kama vile, Liverpool ni ngumu kupotea. Na Spurs walipata shida ya kuchezea mpira sababu ya nguvu kubwa iliyopo Liver hasa kwenye ushambuliaji wakisaidiwa na viungo.

Kiuchezaji ni ngumu pia kuupangua ushirikiano wa Dembele na Wanyama, kwani ni akili nyingi wanatumia kuliko nguvu walizonazo, tabu waliyopata juzi ni uwapo wa Henderson na Wijnaldum ambao wana uwezo wa kutumia nguvu lakini akili pia zinachukua nafasi.

Uzuri wa Henderson msimu huu umechangiwa na uwapo wa Wijnaldum. Mmoja anaposimama dimba la chini kutandaza pasi na kujaribu kupangua ngome, mmoja hukabia dimba la juu na kuhakikisha anasafisha aneo la kiungo cha kati kwa kupokonya, kuingilia pasi na kufanya ‘blocking’.

Nilimtazama Wijnaldum msimu wa 2015 alipokuwa Newcastle United, nikagundua kitu kimoja kizuri kutoka kwake, ni kiungo mjanja kimbinu, hana kasi lakini ni Mdachi mwenye akili ya ziada mchezoni.

Dhidi ya Hull alianzishwa Emre Can badala yake. Mjerumani hakuwa na kasi, alipooza vitu kila dakika, wakapoteza kwa bao 2-0. Hasara.

Je, sasa hivi Liver watakuwa na sababu ipi ya kutomwanzisha Wijnaldum?

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -