Tuesday, November 24, 2020

NASRI AMTETEA WENGER

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal, Samir Nasri, amemtetea kocha Arsene Wenger, akisema ‘haiwezekani kumkosoa yeye’.

Nyota huyo anayecheza kwa mkopo wa muda mrefu Sevilla akitokea Manchester City alikuwamo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Leicester City na kushinda 2-1 dhidi ya mabingwa hao wa England.

Lakini Nasri, aliyefanya kazi na Wenger miaka mitatu ndani ya Emirates, akifunga mabao 27 katika mechi 125 kuanzia mwaka 2008 na 2011, anaona wanaomkosoa kocha wake wa zamani hawafanyi kitu sahihi.

“Huwezi kumkosoa jamaa namna hiyo, haiwezekani. Arsenal ilikuwa klabu kubwa, lakini hata yeye ameifanya kuwa kubwa,” alisema Nasri, akizungumza na Sky Sports.

“Watu wanapaswa kuwa waungwana. Si kwasababu Arsenal hawana mafanikio kwenye ligi useme ni kosa lake, hilo ni kosa la wachezaji uwanjani, ni wachezaji ambao hawapati matokeo mazuri.

“Ni ngumu kwangu kusema kitu kuhusu yeye kwasababu nina deni la vitu vingi kwake. Nimekuja Ligi Kuu England kwasababu yake na nina soka zuri kwasababu yake pia.

“Amenipa kujiamini na kunifanya niwe mchezaji mzuri na wachezaji wengi aliowafundisha wameondoka wakiwa wachezaji wazuri.”

“Sikubali kwamba tatizo ni yeye, kuna matatizo mengi sana Arsenal, wachezaji, bodi inatakiwa kuangaliwa na si Arsene.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -