Sunday, October 25, 2020

Ndalichako ataka wadau kulinda utamaduni

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HERY MBUMA, TUDARCO

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,  Profesa Joyce Ndalichako, amewataka wadau wa masuala ya urithi wa utamaduni kuhakikisha wanaulinda na kuundeleza  kwa manufaa ya vizazi vijavyo kwa sababu urithi huo una manufaa ya moja kwa moja na uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika hotuba yake ya uzinduzi wa kongamano la siku ya urithi wa utamaduni ambayo ilisomwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Moshi Kimizi.

Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni lililokuwa na lengo la kuamsha uelewa kwa umma wa umuhimu wa elimu ya urithi katika maeneo ya mijini.

“Urithi ni kile tulichorithi kutoka zamani, urithi ni kile tunachoishi nacho sasa, urithi ni kile tunachokirithisha kwa kizazi kijacho. Mwisho wa yote urithi  kamwe hauna mbadala, hivyo tuulinde kwa gharama yoyote,” ilisema sehemu ya hotuba ya Profesa Ndalichako.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Urithi cha Ubunifu Majengo Dar es Salaam (DARCH), Aida Mulokozi, alisema lengo la kituo chao ni  kuokoa na kutangaza ubunifu wa kihistoria wa majengo jijini Dar es Salaam na Afrika Mashariki kwa kufanya matamasha ya kitamaduni hivyo  aliiomba Serikali kutunga sheria zitakazohusu utunzaji wa majengo ya kale.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -