Friday, October 23, 2020

NDANDA WAANZA KUPASHA MISULI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MAREGES NYAMAKA


WACHEZAJI wa Ndanda leo wanatarajiwa kuanza mazoezi  kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania, utakaoanza Desemba 27, mwaka huu.

Ndanda wataanza na Simba katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, baada ya kufungwa mabao 3-1 mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Agosti 20, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Mohamed, alisema baada ya mapumziko anatarajia kuendelea na programu ya mazoezi ili kuwajengea ufiti wachezaji wake.

Mohamed alisema ameamua kuwaita wachezaji mapema ili waweze kujiandaa kikamilifu, kwani watakutana na Simba katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili.

Alisema maandalizi mazuri watakayofanya yatawawezesha kuibuka na ushindi kwenye uwanja wao wa nyumbani, aliotoka na ushindi dhidi ya Yanga na Azam katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.

Mohamed alisema pamoja na upungufu mdogo ulioonekana kwenye kikosi chake, anatarajia kufanya usajili katika kipindi cha dirisha dogo la ligi hiyo.

“Tunaingia rasmi kambini na jioni mazoezi yanaanza, kikubwa ni kuwaandaa wachezaji kwa muda mrefu ili tuwaonyeshe Simba ambao wanajivunia rekodi ya kutuchukulia sisi kama wateja wao wa kujipigia na kuchukua pointi tatu.

Ndanda wanashika nafasi ya 10 kutokana na pointi 19, huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 35.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -