Tuesday, November 24, 2020

NDANI YA ETIHAD: ALIYEWEKA MILIONI ASHINDA JIWE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

WASWAZI wakajua jamaa anatania akarudia tena. “Nimesema narudia tena wewe si ni Yanga na mmepewa la mkono, weka jiwe mimi milioni hii hapa tumpe mtu ashike, bao linarudi hili.”

Dogo akaona isiwe nongwa akatoka nje na kuokota jiwe lake akampa kijumbe na Juma yule jamaa mwenye asili ya Kiarabu akakata milioni keshi, mzigo mezani ilipofika dakika ya 80 dogo akaanza kusherehekea kimya kimya mara Kichuya huyoo…shuka nayo.

Mguu wa shingo mguu wa roho ndivyo ndiki hii ilivyokuwa ikipigwa mido ya juu inapiga pasi huku na kutema mate kule wakati mchaka mchaka wa mastreka ulikuwa wa kukata na shoka.

Ngoma hii haikuwa ya kitoto wazee wa mikeka wanaanzaje kuingia kwenye mtego huu, hapa ilikuwa kama unataka kuweka mkeka basi ni kwa staili ya mzigo mezani haijalishi kibindoni umekuja na ngapi.

Msione watu kwenye ndiki kubwa kama hizi wakipoteza fahamu au kupoteza maisha kabisa mkajua labda ni afya zao mgogoro, wengine wanakuwa wameweka bondi mali au wamecheza kamari kutokana na ndiki husika ya siku hiyo, huku uswazi bwana tuachieni wenyewe tumepazoea mbona.

Unaambiwa ndani ya Kibandaumiza mtaani kwetu ilikuwa kimya kama wanandinga wote wamemwagiwa maji si wale wa Kariakoo sokoni wala Jangwani wote walikuwa kimya, hawa wakiwa wamefura kwa hasira baada ya kupigwa la mkono na wale wengine wakiwa na hofu ya kupigwa nyingi kutokana na mashambulizi yalivyokuwa yakiendelea.

Ingawa kimya kilitawala lakini kama kawaida ya uswazi mtu wangu wa nguvu waswazi wa huku kwetu hawakuacha kujifanya ni wataalamu wa benchi la ufundi kwa kulalamikia wachezaji na pengine kuwapanga kana kwamba nao ni makocha bila kujali kama wao walikuwa wakifuatilia kupitia runinga.

Etihad Stadium ndipo alipojichimbia mzee wa Kibandaumiza wiki iliyopita hapa nazungumzia mitaa ya Mbezi juu barabara ya Goba, mmiliki wa hapa ni Hamisi Kizito, wakati inchaji anasimama Hasara Hasan.

Hapa wanaingia watazamaji 90 lakini siku walipokutana watani wa jadi idadi hiyo haikutimia ingawa kwa mujibu wa inchaji Hasara, hao ndio wanandinga wengi zaidi tangu Kibandaumiza hicho kianze.

Ingawa waswazi wengi tumeongeza bei ya kuangalia ndiki ndani ya vibandaumiza vyetu kutoka jero mpaka mia nane, lakini hapa Etihad Stadium imeongezeka maradufu kwani kama huna buku basi utaishia kuchungulia au usije kabisa.

Ingawa sehemu hii haiko mbali sana na baa lakini shabiki haruhusiwi kuingia na kilevi chochote isipokuwa maji na soda pekee ndiyo unaweza kuingia navyo hivyo ukija huku kwetu uswazi ujipange mtu wangu.

Hamisi anasema mwanzoni mwa ligi ndiki zilikuwa zinaneemesha kwakuwa mashabiki wa Manchesta walianza kurudi vibandani kwa fujo pamoja na kwamba walikuwa wakiingia ili kuwaangalia wachezaji wao wapya lakini kingine chama lao lilikuwa likifanya vizuri lakini kwa sasa wameanza kupotea tena baada ya kuvurunda ndiki kadhaa.

Ingawa sehemu nyingi anazoingia mzee wa Kibandaumiza Ligi Kuu ya England ndiyo huangaliwa zaidi, lakini huku uswazi kwetu Mbezi juu ligi ya nyumbani ndiyo mpango mzima, unaambiwa hata ndiki ikipigwa ya Majimaji na Toto watu wanajaa tu ingawa hufikia hadi watu 60 kwa ndiki za nyumbani.

Kwa mujibu wa inchaji Hasara ligi inayofuata kwa kujaza watu ndani ya Kibandaumiza chao ni England halafu baada ya Ubelgiji Hispania ndiyo inafuatia wakati ligi ya Italia imepoteza kabisa msisimko uswazini hapo.

Ebwana eeh, machache tu hayo kutoka pande hizi za Mbezi juu, mimi na wewe tugumiane hapa wiki ijayo mialiko bado inapokelewa ingawa kwa idadi iliyopo sasa nakaribisha mialiko ya mikoani tu, ni kwa muda tu jamaa zangu msikonde.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -