Sunday, November 1, 2020

NDEMLA AJIONDOA SIMBA MAPEMAA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA CLARA ALPHONCE

WAKATI uongozi wa Simba ukisisitiza kutomruhusu kiungo wao, Said Ndemla, kwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna, mchezaji huyo amesema kwa sasa ameamua kuwa mpole lakini ataendelea na mipango yake hiyo baada ya mkataba wake na Wekundu hao kufikia tamati.

Ndemla amekuwa akitakiwa na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Sweden kwa ajili ya kufanya majaribio.

Kama uongozi wa Simba ungemruhusu nyota huyo kwenda kufanya majaribio na kisha kufanikiwa, angeungana na Mtanzania mwingine mshambuliaji Thomas Ulimwengu aliyesajiliwa na AFC Eskilstuna mapema Januari mwaka huu, baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

“Sina jinsi, nimekubali kubaki japo si kwa hiyari yangu, ila nasubiri mkataba wangu umalizike mwaka huu Desemba niondoke, sita saini mkataba mwingine na Simba,” alisema Ndemla.

Alisema hawezi kupimana ubavu na   uongozi wa klabu yake ya Simba kwa kuwa sasa bado ana mkataba na timu hiyo, lakini anaamini bado ana fursa ya kutimiza ndoto zake za kucheza soka la kulipwa barani Ulaya hususani nchini Sweden.

Uamuzi huo wa uongozi wa Simba tayari umekuwa mwiba mchungu kwa mchezaji huyo, kwani kwa mujibu wa wakala wake tayari nafasi yake imejazwa na mchezaji mwingine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -