Thursday, November 26, 2020

Ndemla akubalika sana tu Simba

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa timu ya  Simba, Said  Ndemla, ameanza kuwafurahisha mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kiwango cha hali ya juu alichokionesha katika michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ndemla  ambaye alikuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza, aliweza kung’ara   katika michezo miwili ya ligi hiyo dhidi ya Mwadui na Kagera Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kutokana na uwezo wa kiungo huyo, mashabiki wa Simba,walisema Ndemla ameanza kuwapa raha na kuwasuta waliokuwa wanasema ameshuka kiwango.

Mmoja wa mashabiki hao  wa Klabu ya  Simba, Majid Kassim,  alisema wao wanajua  umuhimu wa Ndemla katika timu yao.

Kassim alisema  viongozi wao pia wanajua  umuhimu wa kiungo  huyo na kuamua kumwongezea mkataba mwingine huku  watani wao Yanga  wakimtaka aondoke na baadaye wamchukue.

Kassim alisema Ndemla ni mchezaji wa Simba kwa muda wote na akiingia uwanjani vitu vyake vinaonekana hata akikaa benchi mwaka mzima.

Naye, Mohamed  Mussa alisema kiwango alichoonesha Ndemla katika michezo miwili aliyochezwa kwa dakika 180 kimewafurahisha  mno.

Mussa alisema kiungo huyo amekuja na moto mkali huku akiwa ameisaidia timu yao kupata ushindi mnono katika michezo hiyo miwili wakiifunga Mwadui mabao 5-0 na baadaye kuichapa mabao 2-0 Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -