Monday, November 23, 2020

NDEMLA AKUMBUSHA VITU VYA MARSHA, CHINA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KIUNGO mahiri wa klabu ya Simba, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, Said Ndemla, mwishoni mwa wiki katika mchezo uliokutanisha timu yake dhidi ya Yanga, alionyesha umahiri mkubwa kwa kufanya vitu adimu.

Mambo mengi aliyokuwa akionyesha kijana huyo, wapenzi wa soka nchini walikuwa wakiviona kutoka kwa viungo ‘mafundi’ wa zamani, Hussein Marsha na Athumani China.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ndemla aliyepangwa kucheza winga ya kulia, alivunja winga hiyo na kucheza kama kiungo mshambuliaji, akisaidiana na kiungo mkabaji, Jastuce Majabvi na Mwinyi Kazimoto. Katika mchezo huo ambao Simba walitawala vilivyo kipindi cha kwanza, Ndemla alionekana kutakata na kucheza vyema, huku akiwalisha vilivyo washambuliaji wake Hamisi Kiiza na Hassan Mussa ‘Mgosi’ kwa pasi za uhakika.

Kati ya vitu vilivyowaacha hoi mashabiki uwanjani hapo, Ndemla alionyesha uwezo wa hali ya juu katika kumiliki mpira, kupiga chenga za maudhi, kupiga mashuti pale alipopata nafasi, lakini kikubwa ikiwa ni uwezo wake wa kupokea pasi za chini na juu kwa ufundi kama walivyokuwa wakifanya Marsha na China enzi zao. Wakati wa enzi zake za kucheza soka miaka ya 1980 mwishoni na 1990 mwanzoni, akichezea klabu ya Pamba ya Mwanza maarufu kama TP Lindanda, Simba na Taifa Stars, Marsha alikuwa akisifika kwa kucheza kandanda la uhakika katika nafasi za kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji.

Licha ya kuwa na umahiri mkubwa wa kumudu kucheza vyema nafasi hizo mbili za kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji, pia ‘fundi’ huyo alikuwa na uwezo wa kucheza nafasi nyingine nyingi kama beki wa kati namba nne, tano na mshambuliaji namba 10. Marsha alimudu kucheza vyema nafasi zote hizo kwa sababu alikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kupiga chenga pale inapohitajika na wakati mwingine kupiga mashuti makali yaliyokuwa yakiwapa kazi ya ziada makipa wa timu pinzani.

Mbali na sifa hizo zote alizokuwa nazo, pia Marsha alikuwa mtaalamu wa kupiga mipira ya adhabu kubwa na ndogo. Alipokuwa akichezea klabu ya Simba na Pamba ya Mwanza, ‘fundi’ huyo alikuwa ni chaguo la kwanza katika upigaji penalti.

Katika dakika 90 za mchezo wowote ilipokuwa inatokea mpira wa kupiga penalti, makocha na wachezaji wenzake walikuwa hawamchagui mtu mwingine zaidi yake kama ilivyokuwa katika upigaji wa penalti tano tano. Ilikuwa ni nadra mno Marsha kukosa kufunga penalti. Hata katika mchezo mmoja ikitokea wamepata nafasi za adhabu hiyo mara mbili, hupewa jukumu hilo kama ilivyokuwa wakati fulani akiwa Simba ambapo aliifunga Pamba mara mbili kwa mikwaju ya penalti katika ushindi wa 2-0.

Kwa upande wake, China naye alikuwa hana tofauti sana na Marsha, kwa sababu alikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kutoa pasi za uhakika, kupiga chenga na kupiga mashuti makali. Kiungo huyo ambaye alikuwa anasifika kwa uchezaji wake huo, aliwahi kuchezea klabu kadhaa nchini zikiwemo Yanga, Simba na timu ya Taifa, Taifa Stars. Kutokana na umahiri mkubwa aliokuwa nao wa kucheza vizuri awapo uwanjani, ilikuwa ni nadra sana kutopangwa katika kikosi cha kwanza.

Alipokuwa akichezea Yanga, China alikuwa ni mmoja wa wachezaji wa kutegemewa kama ilivyokuwa alipojiunga na Simba mwaka 1993. Na kwa jinsi alivyocheza juzi kama ilivyo kwenye mechi nyingine zilizopita, Ndemla huenda akafuata nyayo za Marsha na China iwapo hatabweteka na sifa anazopewa, lakini pia kama atalelewa ipasavyo na klabu yake hiyo ya Msimbazi.

Ikumbukwe kuwa Ndemla ni moja ya zao la timu B ya Simba chini ya kocha Seleman Matola ambapo alianza kuaminiwa na kupewa nafasi kikosi cha kwanza na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Wekundu wa Msimbazi hao, Abdallah ‘King’ Kibadeni na hata Jamhuri Kihwelo.

Na kila alipoingia uwanjani, Ndemla hakuwaangusha makocha wake kwani alifanya kile kilichotarajiwa, kama ilivyokuwa kwa makinda wenzake waliotokea timu B kama Lucian William ‘Gallas’. Kila walipopangwa wakitokea benchi, Ndemla na mwenzake huyo walikuwa wakicheza vizuri na kuonekana kubadilisha mchezo, ikiwa ni pamoja na kiungo huyo kuwachezesha vizuri washambuliaji na wakati mwingine kufunga mabao. Kidogo kidogo, Ndemla baada ya kupata uzoefu, akawa si mtu wa kutokea benchi tena bali ni mchezaji wa kuanza katika kipindi cha kwanza.

Kutokana na ukomavu alionao, kulimfanya mwaka huu kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuchezea timu ya Taifa, Taifa Stars.

Iwapo Ndemla ataendelea kuwa katika kiwango chake cha hivi sasa cha kumudu kucheza vyema nafasi ya kiungo, ni dhahiri atakuwa hazina kubwa kwa Simba na Taifa Stars kwa ujumla na ni wazi atakuwa anawakumbusha wapenzi wa soka nchini vitu adimu vilivyokuwa vikionyeshwa na akina Marsha na China.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -