Tuesday, November 24, 2020

NDEMLA AMEBAKI BONGO KWA MASILAHI YA NANI?

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HASSAN DAUDI

HABARI ya nyota wa Simba, Said Ndemla, kutakiwa kwenda kufanya majaribio katika moja ya klabu za Ligi Kuu Sweden, imeonekana kutawala vichwa vya habari za michezo hapa nchini.

Ndemla alikuwa akitakiwa kufanya majaribio kwa siku kadhaa nchini humo na kama angefuzu basi angelamba mkataba wa kuitumikia timu hiyo.

Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, mpango huo wa Ndemla kukwea pipa na kutua Sweden umepigwa danadana mpaka umepotelea angani.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika, mabosi wa klabu yake ya Simba ndicho chanzo cha kutofanikiwa kwa safari yake ya Sweden mpaka sasa.

Inaelezwa viongozi wa Simba hawapo tayari kumruhusu staa huyo kuondoka na sababu inayowafanya kukwamisha mpango huo inashangaza kweli.

Eti ni kutokana na umuhimu wake kwenye kikosi hicho ambacho kitacheza na Yanga Februari 25!

Kwa maana nyingine, mchezo wa ‘Kariakoo Derby’ utakazozikutanisha Simba na Yanga ndio sababu ya Ndemla kutokwenda kufanya majaribio. Yaani mtanange huo ni muhimu kwa Simba kuliko Ndemla kwenda Sweden kutimiza ndoto zake?

Lakini pia, Ndemla kuisaidia Simba kushinda mechi hiyo dhidi ya mahasimu wao Yanga ni muhimu kuliko mafanikio ambayo soka la Tanzania litayapata ikiwa nyota huyo atakwenda Ulaya.

Hayo yanatokea huku wadau wa michezo nchini wakilalamikia kitendo cha Tanzania kutokuwa na wachezaji wanaocheza nje ya nchi.

Niseme tu kwamba inafikirisha kidogo hasa ikizingatiwa kuwa soka la Bongo liko taabani na sababu kubwa ikiwa ni kukosekana kwa wachezaji wanaocheza nje ya nchi ‘maproo’.

Tanzania imefikia hatua hiyo ya kupuuzia wachezaji wake kwenda kujaribu bahati yao ya kusakata soka la kulipwa nje ya mipaka ya nchi? Sidhani.

Badada ya kuwa kichwa cha mwendawazimu kwa miaka mingi, nilitarajia kuona wachezaji, hasa wenye umri mdogo kama Ndemla wakipewa sapoti kubwa ya kuhakikisha hawakwamishwi kwa njia yoyote pindi wanapobahatika kuitwa nje ya nchi.

Mbali na kutimiza ndoto zao, safari hizo zina faida kubwa kwa timu yetu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwani itaongeza idadi ya mastaa tegemeo, tofauti na hivi sasa ambapo Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ndiyo maproo pekee tunaowategemea.

Ili kuweza kuwa tishio kwenye michuano ya kimataifa, Tanzania inahitaji idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza nje ya mipaka ya nchi ambao watakuwa na ujuzi tofauti kutoka kwa kwenzetu waliopiga hatua katika mchezo wa soka.

Lakini je, kama viongozi wa klabu zetu wakiwamo wa Simba, wanalitambua hilo, kwanini wameendelea kufanya mambo ya ajabu?

Kwa kitendo cha Simba kumzuia Ndemla, natilia shaka utayari wao katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na maproo wengi na hatimaye kuipeperusha vema bendera ya nchi katika michuano ya kimataifa.

Huenda ni kweli mchango wa Ndemla kwenye kikosi cha Simba ni mkubwa lakini Taifa Stars inamhitaji zaidi, tena akiwa katika ‘levo’ nyingine na si hii aliyopo sasa ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kama walivyo Samatta na Ulimwengu, Stars inamtaka ‘Ndemla mpya’, ambaye atakuwa ameiva kutokana na mafunzo ya barani Ulaya.

Kwa mantiki hiyo basi, ni wazi viongozi wa Simba wameangalia zaidi masilahi ya timu yao na kusahau kitu ambacho Stars na Taifa inakihitaji kutoka kwa Ndemla.

Hata hivyo, hii imekuwa ni kawaida ya klabu zenye majina makubwa kuwazuia wachezaji wao pindi wanapoitwa nje ya nchi kwa majaribio au kusajiliwa, hasa pale wanapokuwa na mchango mkubwa kikosini.

Hilo limekuwa likitokea Yanga, Simba na hata Azam wameanza kuiga mfumo huo wa ajabu.

Viongozi wa klabu za hapa nchini wamekuwa wakiweka vikwazo vingi ikiwamo ada kubwa ya usajili, lengo likiwa ni kuwabakisha wachezaji wanaoamini wana umuhimu kwenye vikosi vyao.

Tutakumbuka kuwa kulikuwa na mvutano wa kipindi kirefu kati ya staa Farid Musa na klabu yake ya Azam ambayo ilikuwa ikipiga danadana dili lake la kwenda Hispania lakini mwisho wake aliondoka.

Huenda ni kweli klabu zetu zina haki ya malipo mazuri kwa nyota wao, lakini bado naamini kuna umuhimu mkubwa kwa mastaa wetu kuondoka kwa namna yoyote ile.

Tabia ya viongozi wa klabu zetu kutaja kiasi kikubwa cha fedha ili kukwamisha timu za nje zinazokuja kuchukua wachezaji wetu, haipaswi kuungwa mkono.

Mara nyingi tabia hiyo na ile ya ubabaishaji wa viongozi imekuwa ikizikimbiza klabu zinazokuja nchini kusaka wachezaji, hivyo kukamisha ndoto za Tanzania kujivunia utitiri wa wachezaji wao wanaocheza nje ya nchi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -