Tuesday, January 19, 2021

Ndio mwisho wa ufalme wa Ronaldo Bernabeu?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania

BAADHI ya wachezaji ni wazuri katika kuficha hisia zao mbele ya kamera.

Ni ngumu kutambua kama wana furaha au huzuni wanapokuwa hadharani.

Cristiano Ronaldo si mchezaji wa aina hiyo, atakwambia chochote anachohisi kimemfurahisha au kumkera.

Hivi karibuni, uso wake ulionyesha wazi kukasirishwa na kitendo cha kocha Zinedine Zidane kumwita benchi katika mchezo wa La Liga dhidi ya Las Palmas.

Ronaldo alionyesha wazi kutofurahishwa na uamuzi huo wa Zidane.

Katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi ya wiki iliyopita, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Lakini pia, imeelezwa kuwa Ronaldo alimtolea lugha chafu mama mzazi wa kiungo huyo wa zamani wa Bernabeu na timu ya Taifa ya Ufaransa.

Wachambuzi wengi wa soka wamedai kuwa huenda huo ukawa mwisho wa ufalme wa Ronaldo pale Madrid.

Kwa sasa staa huyo ana umri wa miaka 31 na inaaminika kuwa Ronaldo anaelekea ukingoni.

Kitendo cha Zidane kumpumzisha Ronaldo kimeonekana kuwashangaza wachambuzi wa soka wakidai kuwa inawezekana umuhimu wa nahodha huyo wa Ureno haupo tena.

Akizungumzia uhusiano wake na Ronaldo kuyumba, Zidane alisema: “Kila mchezaji hukasirika anapotolewa uwanjani. Kila kitu kipo sawa, hakuna tatizo. Mimi si mjinga na hata yeye si mjinga.”

Moja kati ya sababu zinazowafanya wachambuzi kuamini kuwa huenda utawala wa Ronaldo ukawa umefikia mwisho pale Bernabeu ni wimbi la majeruhi linalomwandama nyota huyo.

Majeruhi yamemfanya kushindwa kuwa kwenye ubora wake na ni wazi kuwa Ronaldo wa sasa si yule wa miaka miwili iliyopita.

Lakini pia, ikumbukwe kuwa mkali huyo alikosa michezo yote ya maandalizi ya msimu kutokana na majeruhi aliyoyapata akiwa na Ureno katika michuano ya Euro 2016.

Licha ya ukweli kwamba alikuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Madrid msimu uliopita ambapo aliiwezesha timu hiyo kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ni ngumu kumfananisha Ronaldo na Gareth Bale.

Bale raia wa Wales ameonekana kuwa siri ya mafanikio ya safu ya ushambuliaji ya Madrid katika siku za hivi karibuni.

Uwepo wa Bale umeifanya safu ya ushambuliaji ya Madrid kuwa na kasi.

Kwa moto aliouwasha Bale kikosini, wengi wanaamini kuwa ingekuwa hatari zaidi kama staa huyo angekuwa na vita ya maneno na Ronaldo.

Kwa madai ya wachambuzi, huenda Madrid wangekuwa tayari kumfungulia mlango Ronaldo kuliko kumwacha nahodha huyo wa Wales.

Kwa upande mwingine, kama Zidane ataulizwa ni mchezaji gani angependa kubaki naye kikosini kati ya Ronaldo na Bale, bila shaka angemng’ang’ania Bale.

Lakini pia, kuibuka kwa Marco Asensio na Lucas Vazquez, ni pigo jingine kwa mustakabali wa Ronaldo pale Santiago Bernabeu.

Ingawa Ronaldo amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na Madrid misimu kadhaa iliyopita, lakini sasa Zidane hatakiwi kuendelea kumng’ang’ania.

Hata hivyo, wiki chache zilizopita, Ronaldo alikiri mbele ya waandishi wa habari kuwa angependa kumalizia maisha yake ya soka akiwa na Madrid.

Kwa umri alionao hivi sasa na kile alichokifanya Zidane (kumwita benchi katika mchezo dhidi ya Las Palmas), hakuna ubishi kuwa hilo litashindikana.

Ni ngumu kwa Ronaldo kukubali kumalizia soka lake akiwa na nafasi finyu ya kuingia uwanjani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -