Tuesday, January 19, 2021

NDIO MWISHO WA ZAMA ZA ATLETICO?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MADRID, Hispania

Atletico Madrid hawamo tena kwenye mbio za ubingwa wa La Liga na sasa wanapigania kuwemo ‘top four’, kwa mujibu wa mchambuzi wa soka wa Hispania, Terry Gibson.

Real Madrid, Barcelona na Sevilla wakipambana tatu bora, kikosi hicho cha Diego Simeone, kinashika nafasi ya nne kwenye msimamo, huku Real Sociedad wakifuatia ingawa wanafungana na Villarreal kwa pointi.

Wanashika nafasi hiyo ya nne wakiachwa pointi sita na Sevilla waliopo nafasi ya tatu mchambuzi wa Sky Sports, Gibson anaamini kwamba mbio za Atletico kuwania taji La Liga zimefikia mwisho, labda wapiganie mataji mengine kama Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Nafikiri ndio wamefikia mwisho wa mbio za ubingwa. Kwa kweli kwa sasa wanawania ‘top four’,” alisema mchambuzi huyo.

“Nafikiri watafanya vizuri kwenye makombe wanayowania, wako vizuri kwenye Kombe la Mfalme, nafikiri watakuwa tishio tena kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Kwa upande wa La Liga hata hiyo ‘top four’ yenyewe watakuwa na mazingira mabaya, kwani Real Sociedad na Villarreal wanaitaka kwa nguvu zote, pia Athletic Bilbao mbali sana, hivyo Atletico wanapaswa kuwa makini.”

Pia kumekuwa na tetesi kwamba Manchester United wanamtaka mshambuliaji wao, Antoine Griezmann, ingawa Gibson hategemei nyota huyo kuondoka kwenye klabu hiyo ya La Liga.

“Nafikiri Griezmann atabakia Atletico Madrid. Ni klabu kubwa barani Ulaya na wanaweza kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kama kumuuza, basi itakuwa ofa kubwa ndio itawafanya Atletico wampige bei. Ila yote kwa yote ni kwamba msimu huu hawana tena nafasi ya kunyakua taji la La Liga.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -