Friday, October 30, 2020

Ndoa ilivyomsaidia Boateng kuachana na maisha ya anasa 

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania

KWA mashabiki wa soka, Kevin Prince Boateng, si jina geni. Katika klabu zote alizochezea, alijizolea umaarufu kutokana na maisha yake nje ya uwanja.

Akiwa Ligi Kuu England, alizichezea Portsmouth na Tottenham.

Baada ya kutesa Seria A, England na Bundesliga, wakati wa majira haya ya kiangazi ‘brazameni’ huyo alihamishia makazi yake nchini Hispania na kujiunga na Las Palmas ya La Liga.

Hivi karibuni, mkali huyo aliweka wazi jinsi alivyowahi kupoteza sehemu kubwa ya fedha zake kutokana na maisha ya anasa.

Kiungo huyo mshambuliaji alielezea kuwa ni kutokana na mfumo wake huo wa maisha ya kujirusha ndiyo maana kiwango chake kiliporomoka.

Baoteng mwenye umri wa miaka 29, amedai kuwa alitumia muda mwingi kula bata kuliko kuielekeza akili yake uwanjani.

“Siku moja niliamka asubuhi baada ya kutoka kwenye starehe, nikajiangalia kwenye kioo na ndipo nilipojisemea: ‘Nimekwisha.”

Staa huyo raia wa Ghana alisema kuwa alishindwa kutunza fedha zake na hilo lilitokana na umaarufu mkubwa aliokuwa nao.

Boateng alienda mbali zaidi na kudai kuwa alijifunza kuweka fedha akiwa ameshatumia mpunga mrefu.

“Nilipokuwa Tottenham nilikuwa nikipokea fedha nyingi kwa mwezi lakini nilitumia vibaya.

“Magari, nguo na kumbi za starehe ndivyo vitu vilivyonimalizia fedha,” alisema.

Moja kati ya matumizi makubwa aliyowahi kuyafanya nyota huyo ni pale alipotumia Dola 300,000 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania zaidi ya milioni 600.

Lakini pia, alimwaga mpunga huo kununua magari ya kifahari aina ya Lamborghini, Cadillac na Hummer.

Matanuzi hayo yalitokana na mshahara mkubwa aliokuwa akipokea Schalke 04 ambapo alikuwa akikinga pauni 6,000 (zaidi ya shilingi milioni 16) kwa wiki.

Kuna kipindi mashabiki wa wababe hao wa Bundesliga waliwahi kumjia juu wakimtaka kuachana na mbwembwe zake za nje ya uwanja na badala yake kufanya kazi dimbani.

Alichowashangaza wengi ni kitendo cha kuungana na wachezaji wengi wa Ghana kudai posho ya Dola 100,000 wakati wa fainali za Kombe la Dunia, kilikuwa kiasi kidogo sana cha fedha.

Akiwa Spurs, staa huyo aliwahi kuwashangaza mashabiki wa klabu hiyo baada ya kununua pea 80 za viatu.

Ndani ya uwanja, Boateng alikuwa mzigo tu kwani alicheza michezo 14 pekee ya Ligi Kuu England kwa kipindi chote cha miaka miwili alichokaa London tangu aliposajiliwa mwaka 2007.

Lakini sasa, kwa upande mwingine, majeruhi ya mara kwa mara yalimfanya kuikosa michezo mingi ya Spurs.

Katika hali ya kushangaza, akizungumzia sababu ya wimbi la majeruhi ya mpenzi wake, Melissa alisema: “Kuumia kwake mara kwa mara ni kwa sababu huwa tunafanya mapenzi mara saba au 10 kwa wiki.”

“Nina wasiwasi kuwa huenda ikawa ndiyo sababu ya majeruhi yake.”

Hata hivyo, hivi sasa Boateng ameonekana kutulia hasa baada ya kufunga ndoa na mlimbwende Melissa.

Wawili hao walifunga ndoa wakati kipindi ambacho Fainali za Mataifa ya Ulaya za mwaka huu ‘Euro 2016’ zilikuwa zikiendelea nchini Ufaransa.

Boateng ambaye pia aliwahi kuichezea Portsmouth, alinaswa na kamera za mapaparazi na mkewe kwenye moja ya fukwe za Ufaransa.

Ni kipindi hicho ndipo ndugu yake, Jerome Boateng, alikuwa akikiwakilisha kikosi cha Ujerumani kwenye mashindano hayo ya Euro 2016.

Jarome alichagua kuichezea Ujerumani huku Boateng akiamua kuiwakilisha Ghana katika ngazi ya timu ya taifa.

Kwa mara ya kwanza, Boateng aliiwakilisha Ghana katika Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Boateng alizaliwa jijini Berlin na mama yake mzazi, Christine Rahn ni raia wa Ujerumani huku baba yake akiwa ni raia wa Ghana.

Mdogo wake, Jarome Boateng yuko Bundesliga akikipiga katika klabu ya Bayern na hajawahi kuishi Ghana.

Boateng aliwahi kumpa talaka mke wake wa kwanza aliyefahamika kwa jina la Jenny. Mpaka wanaachana, wawili hao walikuwa na mtoto mmoja wa kiume, Jermaine-Prince.

Kwa upande wake, mdogo wake Jarome aliwahi kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Sherin Senler na walibahatika kupata watoto wawili wa kike, Soley na Lamia ambao ni mapacha.

Baadaye wawili hao waliachana huku sababu ikitajwa kuwa Boateng alikuwa akitoka kimapenzi na wasichana wengine.

Hata hivyo, walirudisha uhusiano wao wa kimapenzi Novemba mwaka 2013.

Boateng alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimalavidavi na mwanamitindo, Gina-Lisa Lohfink, ingawa wawili hao walikanusha taarifa hizo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -