Monday, January 18, 2021

NEEMA YA UDHAMINI YAIANGUKIA SINGIDA UTD

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

singida

ZAINAB IDDY NA TIMA SIKILO

KLABU ya soka ya Singida United imeendelea kupata neema ya udhamini kujiimarisha na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya YARA, inayosambaza mbolea nchini.

Mkataba huo, ambao ulisainiwa jana, una thamani ya zaidi ya Sh milioni 250 kwa mwaka na bado kuna wadhamini wengine watatu ambao watatambulishwa muda wowote.

Kikosi cha Singida, ambacho kitashiriki Ligi Kuu msimu ujao, kimepata bahati ya kupata wadhamini, kwani mbali na Kampuni ya YARA, kuna Kampuni ya SportPesa, iliyoingia mkataba wa Sh milioni 250 kwa mwaka mmoja.

Akizungumza kwenye hafla ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Alexandre Macedo, alisema wanahusika na masuala ya kilimo, hivyo makubaliano ya Singida United kuwa na nembo ya alizeti yamewavutia kufanya nao kazi.

“Mbali na kujihusisha na kilimo, pia mimi binafsi ninapenda soka, hivyo nikaona si vibaya kufanya nao kazi,” alisema Macedo.

Naye Mkurugenzi wa klabu ya Singida United, Festo Sanga, alisema udhamini waliopata utazidi kuwafungulia njia, kwani licha ya kuwa na wadhamini watano hadi sasa, kuna wengine watatu watamalizana nao muda wowote.

“Tumejipanga ili timu yetu isikumbwe na ukata, ndiyo maana tunahangaika kila sehemu kuhakikisha tunapata wadhamini zaidi ya saba ili tucheze soka la ushindani, kwani mpira sasa ni biashara,” alisema Sanga.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm, alisema udhamini waliopata ni chachu ya kikosi hicho kufanya vizuri msimu ujao.

“Namefurahi kwa sababu baada ya kupata mafanikio  Yanga nimepata fursa nyingine ya kuendeleza mafanikio hayo kwa Singida United,” alisema Pluijm.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -