Friday, November 27, 2020

NEW HABARI, LORD BADEN WAANZA KUWASAKA AKINA SAMATTA WAPYA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SHARIFA MMASI

WANAFUNZI waliomaliza darasa la saba mwaka huu ambao wana vipaji mbalimbali, wamepata zali la mentali kwa kugharamiwa masomo yao ya sekondari bure katika Shule ya Lord Baden Memorial iliyopo Bogamoyo, mkoani Pwani.

Shule hiyo inayoongozwa na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu, imeamua kufanya hivyo kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza michezo nchini pamoja na taaluma.

Kwa mwaka huu, mpango huo wa aina yake umepewa sapoti ya hali ya juu na Kampuni ya New Habari (2006) Limited, wazalishaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, Rai pamoja na The African.

Kwa mujibu wa mratibu wa mpango huo, Michael Maurus, tayari mchakato wa kuwapata watoto wenye vipaji umekamilika na unanza rasmi leo hii.

Alisema mchakato huo ulianza takribani miezi mitatu iliyopita kwa wazazi kujaza fomu zilizotolewa kwenye magazeti ya Bingwa na Dimba na kuzituma ofisi za New Habari, ambapo mpaka sasa tayari watoto zaidi ya 70 wamethibitisha kushiriki.

“Tumefurahi kuona si wazazi wa Dar es Salaam pekee waliochangamkia fursa hii, bali hata maeneo ya vijijini ya mikoani kama vile Simiyu, Tabora, Kigoma, Lindi, Ruvuma, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Geita, Pwani, Morogoro na kwingineko kuonyesha jinsi Watanzania walivyo na mapenzi ya watoto wao kuona wanafanikiwa kupitia vipaji vyao,” alisema Maurus.

Alisema mchakato wa kupima uwezo wa kila mtoto utafanyika kwa siku tatu, yaani kuanzia Jumapili ya Januari mosi hadi Januari 3, mwakani pale Lord Baden hivyo kuwataka wazazi kufika shuleni hapo siku mbili za mwisho ili kushuhudia vipaji vya watoto wao.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Matangazo na Masoko wa New Habari, Michael Budigila, alisema kuwa wanafarijika kuwa sehemu ya mpango huo wakiwa kama miongoni mwa wadau wa michezo na elimu kwa ujumla, hapa nchini.

“New Habari kama chombo cha habari, ni wadau muhimu mno wa masuala ya elimu, sanaa na michezo, hivyo kujikita kwetu katika mpango huu ni moja ya sehemu ya kutekeleza majukumu yetu kwa jamii,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Lord Baden School, Iddi Kipingu, alisema kuwa mpango huo ni sehemu ya mkakati wa shule yake kuwalea watoto kielimu, lakini pia kuheshimu vipawa vyao.

“Kupitia mpango huu, tunaamini tutakuwa tumetoa mchango wetu wa kuvumbua na kuviendeleza vipaji vya vijana wetu ili viweze kuwa tegemeo la Taifa kwa siku zijazo,” alisema Kipingu aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Juu ya suala zima la elimu, Kipingu alisema pamoja na michezo na sanaa, watoto watakaopata nafasi ya kusoma Lord Baden, watajengwa vilivyo katika masomo mengine ya darasani, lakini msisitizo zaidi ukiwekwa kwenye lugha tofauti kama Kichina, Kifaransa na Kiingereza.

“Kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumewapanulia wigo wa kueleweka kokote watakakokwenda kusaka maisha kupitia vipaji vyao, kwani watakuwa na uwezo wa kuzungumza lugha mbalimbali kwa ufasaha kabisa,” alisema Kipingu, mmoja wa wadau.

Ifahamu Lord Baden

Lord Baden ni miongoni mwa shule bora katika kukuza, kuendeleza na kuibua vipaji vya michezo.

Somo la michezo limekuwa ni sehemu ya lazima katika shule hii na linafundishwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Wanafunzi kuanzia kidato cha pili na cha nne hutumia somo hili kwa kufanyia mitihani ya Taifa ikiwa ni sehemu ya somo la ziada, lakini wanafunzi wa kidato cha nne linawasaidia kujiongezea alama “credit” katika mitihani yao ya Taifa ambapo imewasaidia wengi wao kuweza kuendelea na kidato cha tano.

Shule hii ina mchanganyiko wa michezo mbalimbali ikiwamo mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana, mpira wa pete (Netball), riadha, mpira wa kikapu, pamoja na michezo mingine.

Michezo imekuwa ikiwajenga wanafunzi wa shule hii ya Lord Baden kwa kuwawezesha kupata mbinu mbalimbali za michezo kutokana na kuwa sehemu ya somo linalofundishwa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.

Ufanisi wake

Kuanzia mwaka 2009 hadi 2011, shule hii ilikuwa na spoti academy iliyokuwa ikiendeshwa na Wafaransa na ikafanikiwa kuwapata baadhi ya wachezaji wanaofanya vizuri katika klabu mbalimbali nchini ikiwamo Simba, Azam,Toto FC, Mtibwa Sukari na Moro United.

Baada ya kuachana na academy ya Wafaransa, Kipingu alianzisha academy nyingine iliyopewa jina la Kipingu Twaweza iliyopo shuleni hapo ambayo ilichukua jukumu la kutunza vijana chini ya miaka 14 hadi 17.

Kwasasa academy hii imejiunga na academy ya Afrika Kusini ya Santos ili kuweza kuendelea kuibua vipaji mbalimbali.

Baadhi ya mafanikio kimichezo

Katika timu ya wasichana walifanikiwa kushiriki mashindano yaliyokuwa yakidhaminiwa na Kampuni ya Simu ya Airtel (Airetl Competition), yaliyofanyika nchini Nigeria ambapo waliweza kutwaa ubingwa wa Afrika kwa wasichana.

Upande wa mpira wa kikapu

 Shule hii iliweza kufanya vizuri mwaka 2014 ambapo waliweza kuwa mabingwa Afrika Mashariki na Kati katika mashindano yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mbali na hilo, katika mashindano ya watoto wenye umri chini ya miaka 15 yliyomalizika Oktoba mwaka huu, Lord Baden iliibuka kidedea huku mchezaji wake Hossam Kitwana akitajwa mchezaji bora wa mwaka (MVP).

Tukiangukia riadha

Shule hii ilikuwa na wanariadha na watupaji ambapo katika upande huo iliibuka na medali ya dhahabu kwenye timu ya Taifa.

Cha kujivunia

 Wamekuwa wakidumisha michezo pamoja na taaluma kwa muda wote, kukuza vipaji vinavyoendelea kufanya vyema mpaka sasa wakiwamo Hassan Kessy, Omega Cheni, Lambele Jerome aliyewahi kuchezea timu ya Moro United na Simba chini ya miaka 20, Adiba Adam wa timu ya Simba, Maka Shaban aliyechezea timu ya Mafunzo Zanzibar.

Pia walifanikiwa kuwafunza Edward Gabriel aliyekuwa katika timu ya Simba na kwenda timu ya Toto FC ya Mwanza ambapo hivi sasa anachezea timu ya Kagera Sukari.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -