BARCELONA, Hispania.
NYOTA wa Barcelona, Neymar ameweka wazi kwamba ataendelea kubakia kwenye klabu hiyo pamoja na kuhusishwa na klabu mbalimbali kama Manchester United. Nyota huyo wa Brazil alikuwa akifukuziwa na kocha wa Man United, Louis van Gaal majira haya ya kiangazi.