Thursday, December 3, 2020

NEYMAR NI ZAIDI YA RONALDO NA RONALDINHO

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

UNAPOKUJA mjadala wa ni akina nani wanastahili kuitwa wachezaji bora Brazil, Ronaldo na Ronaldinho wanahitaji heshima kubwa zaidi ya kutajwa pekee kwenye orodha hiyo.

Sasa wamekwishatundika daluga, wakiacha kumbukumbu ya uwezo wao wa ‘Joga Bonito’ (soka la kuvutia).

Wawili hao walikutana pamoja kujibu maswali ambayo wengi walikuwa nayo, wakihojiwa na televisheni ya TV Globo wakiwa wameshika karatasi zenye namba zao, mfano Ronaldo alishika kikaratasi kilichoandikwa ‘R9’ na ‘R10’ kwa Ronaldinho.

R9 alikuwa wa kwanza kujibu swali kwamba nani alikula bata zaidi katika wachezaji wa kikosi cha Brazil cha miaka 2000 ambao walibeba Kombe la Dunia 2002?

“Brazil tunapenda bata, hilo liko wazi,” alisema Ronaldo. “Mimi ndio nilifunika kwa kula bata.”

Kisha wachezaji hao waliulizwa nani alikuwa mkali zaidi wakiwa Nou Camp wakiichezea Barcelona, ambapo wote wamekipiga La Liga wakati wa zama zao.

Safari hii, Ronaldinho ndiye  aliibuka kidedea kutokana na kile ambacho alikisema baada ya kukaa Barca kwa miaka mitano.

“Ilikuwa kawaida kwa sababu alikaa muda mwingi zaidi kuliko mimi, nilicheza mwaka mmoja pekee,” alieleza Ronaldo.

Walipoulizwa kuhusiana na nyota wa Brazil anayekipiga sasa Barcelona, Neymar, ambaye analinganishwa na nyota hao wawili kwa klabu yake na timu yao ya taifa, Ronaldo, alisema: “Neymar ana vitu adimu ambavyo Brazil tunapenda, ujasiri, uwezo wa kukokota. Kukimbilia mpira.”

Ronaldo na Ronaldinho wamefunga mabao mengi bab kubwa, lakini kuna mjadala ni wapi na lini na lipi bao bora kwao.

Kila mmoja alizungumzia bao lake, ambapo Ronaldo alianza na kuzungumzia bao lake la juhudi binafsi dhidi ya Compostela, huku Ronaldinho akikumbushia lile alilofunga dhidi ya Real Madrid kwenye mechi ya ‘El Clasico’ mwaka 2005.

“Bao langu la pekee, bao la maisha yangu ya soka ni lile nililofunga dhidi ya Compostela,” alisema Ronaldo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -