Wednesday, January 20, 2021

NGAO YA JAMII KESHO… MASHABIKI SIMBA, YANGA WAJIANDAE KISAIKOLOJIA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MARIAM SHABANI NA REHEMA SIMON (TUDARCO)

PAZIA la msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa rasmi kesho kwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga, utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ligi hiyo, inayodhaminiwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania, inatarajiwa kuanza Agosti 26, mwaka huu, kwa timu mbalimbali kuonyeshana kazi kwenye viwanja tofauti.

Yanga ndio wanaoshikilia ubingwa wa ligi hiyo, inayoshirikisha timu 16, wakiwa wamebeba kombe kwa misimu mitatu mfululizo.

Timu hiyo, yenye maskani yake katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, ni miongoni mwa zinazopewa nafasi kubwa ya kubeba kombe la msimu ujao.

Hata hivyo, timu hiyo itakabiliwa na upinzani wa aina yake kutoka kwa timu nyingine, zaidi wakiwa ni watani wao wa jadi, Simba.

Mbali ya Simba, timu nyingine zenye uwezo wa kutwaa ubingwa wa Bara ni Kagera Sugar walioibuka washindi wa tatu msimu uliopita, Azam FC na Singida United chini ya kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm.

Mtibwa Sugar, Mbeya City, Tanzania Prisons, Lipuli FC na nyinginezo, pia zina uwezo wa kutoa changamoto ya aina yake katika suala zima la kupigania ubingwa wa ligi hiyo ya Bara.

Ukiachana na timu hizo, mashabiki wa Simba na Yanga wameonekana kujiamini mno kuwa timu zao ndizo zenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa na kukata tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu wa 2018/19.

Hilo linatokana na kile kinachoonekana imani ya ubora wa vikosi vyao, hasa baada ya usajili uliofanywa na timu zao msimu huu.

Simba, ambao ndio walioanza kutikisa katika dirisha la usajili kwa kutangaza kuwanasa wachezaji nyota nchini, wakiwamo kutoka Yanga, wanaonekana kuwa na matumaini makubwa ya kutawala soka la Tanzania msimu ujao.

Baadhi ya wachezaji wanaowapa Simba jeuri ni kiungo Haruna Niyonzima, aliyekuwa Yanga, kipa Aishi Manula, kiraka Erasto Nyoni, beki wa kulia Shomari Kapombe na mshambuliaji John Bocco, wote kutoka Azam.

Pia, wapo Jamal Mwambeleko na Emmanuel Mseja wote kutoka Mbao FC, Yusuph Mpilili (Toto Africans), Said Mohammed (Mtibwa Sugar), Emmanuel Okwi (SC Villa ya Uganda), Mghana Nicholas Gyan na wengineo.

Simba wanaamini kwa kuwa na wachezaji hao wapya pamoja na wale wa zamani, wanaoongozwa na Jonas Mkude, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Jjuuko Murushid, Method Mwanjali, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Muzamir Yassin, Laudit Mavugo na wengineo, hakuna wa kuwazuia msimu ujao katika mbio za ubingwa.

Kwa upande wao, Yanga wanawatambia Ibrahim Ajib kutoka Simba, Rafael Daudi (Mbeya City), kiungo mkabaji kutoka Kongo, Pappy Kabamba Tshishimbi, kipa Mcameroon Youthe Rostad (African Lyon), Gadiel Michael (Azam), Ramadhan Kabwili na wengineo.

Mashabiki wa Yanga wanaamini kwa kuwa na wachezaji hao, hasa Ajib, hakuna wa kuwazuia kutetea ubingwa wao wa Bara kwa mara ya nne.

Lakini wakati mashabiki wa wakongwe hao wa soka wakiwa na matumaini kibao, ni wazi kuwa wanatakiwa kujiandaa kisaikolojia, kwani katika soka, lolote linaweza kutokea kesho na kwenye mechi zao zinazofuata za Ligi Kuu Bara.

Pamoja na tambo zao kutokana na usajili uliofanywa na timu zao, iwapo waamuzi watachezesha kwa kufuata sheria zote 17 za soka, huku Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likitimiza majukumu yake bila upendeleo wowote ule, watu wa Simba na Yanga wasijeshangaa kombe likitua katika mikoa ya Mbeya, Singida, Kagera, Morogoro, Iringa au kwingineko.

Kama ilivyojionyesha msimu uliopita, hasa Kagera Sugar, iwapo timu za mikoani zitaamua kukaza na kukataa kuwa vibaraka wa Simba na Yanga, zinaweza kufanya maajabu na kutwaa ubingwa wa Bara kama ilivyokuwa kwa Coastal Union, Mtibwa Sugar, Pamba FC, Tukuyu, Lipuli na nyinginezo za mikoani zilizowahi kufanya hivyo kwa miaka tofauti.

Ifahamike kuwa, Simba na Yanga zimesajili wachezaji wenye majina makubwa, ambao wanaweza kutoa matokeo tofauti kabisa na matarajio ya mashabiki wao.

Na kwa kuwa wakongwe hao wa soka nchini wanakutana kesho, ni nafasi ya kipekee kwa mashabiki wa timu hizo kujipima kama wanaweza kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kwa vikosi vyao, zaidi ikiwa ni nyota wao wapya kushindwa kufanya kile walichokitarajia.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -