Wednesday, October 28, 2020

‘NGASSA, AJIB DUGU MOJA’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA TIMA SIKILO

Nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa na Ibrahim Ajib, wameelezewa kuwa na udhaifu unaolingana ambao ni wa kutokuwa fiti kwa dakika zote 90.

Hayo yamesemwa jana na kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, akijibu hoja za mashabiki wao ambao wamekuwa wakilalamikia kitendo cha Ngassa kutopewa dakika zote 90 za mechi zao mbalimbali.

Katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi, Ngassa pamoja na kufunga bao la pili la Yanga, alitolewa dakika ya 61 na nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke.

Kitendo cha Ngassa kutolewa kilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa Yanga wakiamini nyota wao huyo bado alikuwa na uwezo wa kukinukisha.

Akijibu hoja za mashabiki wao, Zahera alisema: “Ngassa ni kama Ajib, tena yeye ni zaidi ya Ajib. Hawezi kucheza kwa kasi inayotakiwa kwa dakika 90. Akitaka kucheza kwa muda wote, avumilie kuteseka mazoezini.”

Alisema kwa akili ya mpira aliyonayo Ngassa, angekuwa na pumzi ya kutosha, angekuwa tishio kama ilivyo kwa Ajib ambaye ametokea kuwa kipenzi cha Wana-Yanga kutokana na vitu vyake adimu uwanjani.

Kikosi cha Yanga kwa sasa kinaonekana kuwa na kasi ya ajabu Ligi Kuu Bara, kikiwa hakijapoteza mchezo wowote kati ya saba waliyocheza, ikipata sare moja tu dhidi ya Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -