Tuesday, October 27, 2020

NGASSA KUJIUZA UPYA KWA AZAM

Must Read

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha...

WINFRIDA MTOI NA AGAPE GODRICH (DSJ)


MRISHO Ngassa akiwa na kikosi chake kipya cha Mbeya City, anatarajia kushuka dimbani kesho kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Ngassa amejiunga na Mbeya City kipindi cha usajili wa dirisha dogo akitokea Fanja FC ya Oman na kwamba wapenzi wa soka nchini watakuwa na shauku kubwa kuona nyota huyo anafanya nini kesho ili ‘kuitia njaa’ Azam na timu nyinginezo za Ligi Kuu Bara.

Tangu Ngassa amejiunga na Mbeya City, huo utakuwa mchezo wake wa kwanza kucheza Dar es Salaam tangu alipoondoka katika vikosi vya Yanga, Azam na Simba alizozichezea kwa nyakati tofauti.

Aidha, winga huyo amekuwa nje ya ligi ya Tanzania kwa zaidi ya msimu mmoja na nusu baada ya kujiunga na klabu ya Free State Stars ya Afrika Kusini kabla ya baadaye kutua Fanja FC.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Katwila: Sitaidharau Mbeya City

NA VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Ihefu, Zuberi Katwila, amesema hawaraidharau  Mbeya City...

Kocha apokea kipigo kwa shingo upande

 NA  VICTORIA GODFREY KOCHA wa timu ya Mwadui, Khalid Adam, amesema amesikitishwa na kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa...

KMC kumaliza hasira kwa Gwambina

NA WINFRIDA MTOI BAADA ya kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Yanga, kocha msaidizi wa timu ya Manispaa...

Tshishimbi atambulishwa kuvaa uzi wa AS Vita

NA MWENDISHI WETU KIUNGO wa zamani wa timu ya  Yanga, Papy Tshishimbi, ametambulishwa katika kikosi cha AS Vita ya...

Kaseja: Hatukuwa dhaifu kwa Yanga

NA ZAINAB IDDY NAHODHA wa timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),  amesema  hawakuwa dhaifu mbele ya Yanga, licha ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -