Tuesday, October 27, 2020

NGOMA AFUMUA KIKOSI YANGA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

HUSSEIN OMAR NA CLARA ALOPHONCE

PAMOJA na kikosi cha Yanga kukumbwa na janga la wachezaji wake wengi kuwa na adhabu za kadi za njano, lakini kocha msaidizi, Juma Mwambusi, amesema hawana wasiwasi na tatizo hilo.

Mwambusi amesema wana kikosi kipana cha kuwafanya wasiwe na hofu na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Stand United, utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika jana asubuhi katika Uwanja wa Chuo cha Polisi kilichopo Kurasini, Dare es Salaam, ambapo benchi la ufundi lilianza kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita.

Programu ya mazoezi yao ya jana iliongozwa na kocha George Lwandamina, ilianza kwa wachezaji kugawanywa kwenye makundi matatu na kuwafundisha mbinu za kukaba na kumiliki mpira kwenye mazingira magumu ya kuzungukwa na adui.

Pia Lwandamina aliwapa mbinu za kufunga kwa washambuliaji wake, Obrey Chirwa, Anthony Matheo na winga Juma Mahadhi.

Baada ya mazoezi hayo, alianza kukinoa kikosi chake kitakachovaana na Stand bila ya nyota wake muhimu na kuwagawa wachezaji katika timu mbili.

Kikosi cha kwanza kilikuwa na Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Andrew Vicent, Justin Zullu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Obrey Chirwa, Juma Mahadh na Emanuel Martin.

Wachezaji hao waliokuwa wakinolewa kwa ajili ya kuziba mapengo ya Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Juma Makapu na Kelvin Yondani, ambao wanatumikia adhabu hiyo ya kadi mbili za njano.

Akizungumza na BINGWA jana, Mwambusi alisema Yanga ina kikosi kipana chenye wachezaji wazuri wanaoweza kuipa timu matokeo mazuri, hivyo hawana wasiwasi katika kuwatumia.

“Wachezaji wetu watano wana kadi za njano. Lakini Yanga ina kikosi kipana, wachezaji wote ni muhimu. Ni uamuzi wetu sisi benchi la ufundi tumtumie mchezaji yupi na yupi tusimtumie,” alisema Mwambusi.

Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha Mbeya City na kuipa mafanikio makubwa, alitolea mfano  na kusema kuwa, kukosekana kwa Donald Ngoma katika kikosi hicho kwenye mechi kadhaa, pengo lake halikuiathiri timu hiyo kwani liliweza kuzibwa vizuri na wachezaji wengine.

“Kwa taarifa yako alikosekana Ngoma, lakini umeona timu imecheza na imepata matokeo mazuri. Pengo limezibwa vizuri,” aliongeza Mwambusi.

Kwa sasa Ngoma amesharejea mazoezini baada ya kusumbuliwa na majeraha, jana asubuhi alianza mazoezi na wenzake yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Ngoma ambaye hakuwa fiti baada ya kupata majeraha ya goti katika michuano iliyomalizika mwezi uliopita ya Kombe la Mapinduzi, jana alipewa progamu ya mazoezi mepesi kwa ajili kuuweka sawa mwili wake.

Kuumia kwake kulimfanya akose michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Majimaji ya Songea na Mwadui FC.

Daktari wa timu hiyo, Edward Bavu, aliliambia BINGWA kuwa Ngoma sasa yupo fiti kwa asilimia 100 na kwa mujibu wa meneja Hafidh Salehe, nyota huyo atacheza katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Stand United.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -