Tuesday, November 24, 2020

NGOMA APIGA TIZI LA KIBABE, BOSSOU KUREJEA LEO KUIKABILI AZAM

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, watakuwa ‘full’ nondo kuelekea mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi hiyo dhidi ya Azam, unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kutokana na wachezaji wao muhimu kurejea kikosini.

Wachezaji hao tegemeo ni mshambuliaji, Donald Ngoma, ambaye jana aliungana na wenzake mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi hiyo, wakati beki wa kati wa kikosi hicho, Vicent Bossou, anatarajiwa kurejea leo na kuungana na wenzake.

Bossou atawasili leo akitokea nchini Misri, ambako alikuwa akiiwakilisha timu yake ya Taifa ya Togo kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Misri.

Katika mchezo huo wa kirafiki wa kikosi hicho cha Bossou, kilipokea kichapo cha mabao 3-0 na wenyeji wao hao, kwenye Uwanja wa Borg El Arab nchini Misri.

Ngoma ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya goti na kuwa nje kwa takribani miezi mitatu kabla ya kurejea na kuumia tena, sasa yuko fiti na amerejea mazoezini jana.

Katika mazoezi hayo, Ngoma alianza mazoezi peke yake kuanzia saa 9:00 alasiri, akizunguka uwanja hata wachezaji wenzake walipofika yeye aliendelea kujifua.

Kurejea kwa wachezaji hao wawili, Bossou na Ngoma, kutaifanya Yanga kuendelea kuwa imara kwenye safu ya ulinzi na kuongezeka makali kwa upande wa ushambuliaji.

Wachezaji wengine waliokuwa majeruhi na jana walirejea kikosini ni pamoja na Juma Abdul, Thaban Kamusoko, Justin Zulu, huku mlinda mlango, Deogratius Munishi ‘Dida’, Simon Msuva na Andrew Vicent ‘Dante’ wakipewa mapumziko kutokana na kuwamo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Akizungumza na BINGWA, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alithibitisha kurejea kwa Bossou na kusema ataingia moja kwa moja kambini kuungana na wenzake.

“Kikosi kipo vizuri, wachezaji wengi waliokuwa wamerejea kikosini kama Ngoma, Kamusoko, Zulu na Abdul, huku Bossou akitarajiwa kuingia kesho (leo) kuiwahi mechi ya Azam ambapo akifika ataingia kambini moja kwa moja kuungana na wenzake,” alisema Hafidh.

Yanga inahitaji ushindi kwenye mchezo huo ili kuweza kuwashusha mahasimu wao Simba waliko, ambapo kama mabingwa hao watetezi watafanikiwa kushinda mechi hiyo watafikisha pointi 56 huku ikiwaombea mabaya Simba iteleze dhidi ya Kagera Sugar hapo Jumapili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -