Friday, November 27, 2020

NGOMA, BOSSOU, NIYONZIMA, DIDA, MWINYI ‘BYE BYE’ YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA WAANDISHI WETU,

KIPIGO walichokipata Yanga cha mabao 2-1 kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba, kimeacha vumbi ndani ya klabu hiyo ambapo imeelezwa baadhi ya wachezaji wapo mbioni kutimuliwa.

Yanga walitambiwa na Simba katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mbaya zaidi ikiwa hivyo huku Wekundu wa Msimbazi wakiwa pungufu baada ya beki wao, Javier Bokungu, kutolewa kwa kadi nyekundu mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Wachezaji wanaotajwa kuwa katika mpango wa kufukuzwa muda wowote kuanzia sasa, ni wale wanaodaiwa kucheza chini ya kiwango, kwa mujibu wa habari zilizodakwa na BINGWA kutoka ndani ya klabu hiyo.

Wanaotajwa ni kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, beki wa kushoto, Haji Mwinyi, kiungo mshambuliaji, Haruna Niyonzima, huku Donald Ngoma na Vincent Bossou wakiingizwa katika kundi hilo kutokana na kitendo chao cha kukataa kucheza mchezo huo wa Jumamosi iliyopita.

Nyota hao watano ambao wamebakiza miezi michache kabla ya mikataba yao kumalizika pamoja na mkakati wa kutoongezewa mikataba, wanaweza kuwa nje ya programu za Yanga katika mechi zote zijazo ili kutoa nafasi kwa wale wanaojitambua na kuheshimu majukumu yao kupewa nafasi.

Kwa upande wao pamoja na uwezo wao uwanjani, Ngoma na Bossou, huenda wasiongezwe mikataba kutokana na vitendo vyao vya kugomea mchezo huo dhidi ya Simba, lakini pia wakidaiwa kuwa wasumbufu wa mara kwa mara pale inapotokea wanacheleweshewa mishahara yao.

Taarifa kutoka Yanga zinadai kuwa kabla ya mchezo huo wa Jumamosi, daktari wa kikosi hicho, Samweli Bavu, aliliambia benchi la ufundi kuwa Ngoma alikuwa fiti kuwavaa Simba kwani alishapona majeraha yaliyokuwa yanamkabili ila Mzimbabwe huyo ndiye aliyeweka mgomo.

Kwa upande wake, Bossou ameelezwa kutokuwa na tatizo lolote ila alikataa kuingia uwanjani kama mgomo kwa kuwa alicheleweshewa mshahara wake.

Niyonzima, Mwinyi na Dida wanashutumiwa na mashabiki wa timu hiyo kwa kudaiwa kucheza chini ya kiwango katika mpambano huo na ndio waliochangia kwa kiasi kikubwa Simba kuibuka na ushindi.

Alipoulizwa juu ya mpango huo wa kuwatimua nyota wao hao na hatimaye kuunda jeshi jipya, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Paulo Malume, alisema kuendelea au kutokuendelea kuichezea Yanga kwa nyota hao kutategemea na ripoti ya kocha wao, George Lwandamina, atakayoikabidhi kwa viongozi.

“Sasa hivi wote wamebakiza miezi michache kumaliza mikataba yao, kwa sasa siwezi kusema lolote zaidi ya kusubiri ripoti ya mwalimu kisha tufanye maamuzi magumu,” alisema Malume.

Alisema wamesikitishwa mno na kitendo cha timu yao kufungwa mabao 2-1 na Simba, wakati walishakuwa mbele kwa bao 1-0, huku wapinzani wao hao wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja.

“Tumefungwa sawa tumekubali, inauma, lakini nawaomba mashabiki wetu watulie kwani kimya kingi kina mshindo, wasione tumekaa kimya wakadhani tumepuuzia matokeo haya, kuna vitu tunafuatilia ili kufanya maamuzi magumu.

“Ni matokeo magumu sana kuyakubali, lakini kimsingi bado tuna mechi nyingi mkononi, ni suala la kujipanga tu, hakuna kitakachoharibika kuelekea mbio za ubingwa mwaka huu,” aliongeza Malume.

Previous articleUPENDO KUSHINDA UFAHAMU
Next articleKWANINI KICHUYA TU?
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -