Wednesday, November 25, 2020

Ngoma, Kamusoko hawapo salama Yanga 

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

WAKATI Yanga ikimshusha kocha Mzambia, Geogre Lwandamina ambaye atakuwa akisaidiana kazi na Han van Pluijm, ujio huo umeelezwa kuwaweka njiapanda nyota kadhaa ndani ya kikosi hicho.

Lwandamina tayari amejiuzulu kuifundisha Zesco United ambayo aliifikisha hatua ya nusu fainali kwenye Klabu Bingwa Afrika mwaka huu, anatua kuanza kazi rasmi kwenye kikosi hicho cha Wanajangwani.

Kwa rekodi zake kwa kipindi chote alichokuwa mkuu wa benchi la ufundi la Zesco, ni rahisi kutabiri kuwa Yanga wamelamba dume kwa kumchukua Lwandamina.

Lakini ujio wake unaweza kuwa kilio kwa baadhi ya wachezaji kwenye kikosi hicho alichopewa sharti la kuifikisha Yanga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo anatakiwa kukiongezea nguvu kikosi anachoachiwa na Pluijm.

Sharti hilo alilopewa ni wazi, Lwandamina atalazimika kufanya usajili wa uhakika hapo Januari, hivyo nyota kadhaa wanaweza kuondoka kwenye kikosi hicho.

Kwa kawaida kila kocha ana mfumo na tabia zake, hivyo anapobadilishwa na kuletwa mwingine maana yake ni kwamba, wanaanza upya hasa kwenye suala nzima la usajili.

Kama unakumbuka, ujio wa Mbrazil, Marcio Maximo ndani ya kikosi cha Yanga, uliwaondoa nyota kadhaa kwenye kikosi hicho kama Mganda, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbagu ambapo alikuja na nyota wake, Andrey Coutinho, Santos Santana Jaja na baadaye katika usajili wa dirisha dogo alimleta kiungo mkabaji, Emerson de Oliveira Neves Roque, akitaka kumtosa Mbuyu Twite.

Hivyo hata Lwandamina atakuja na falsafa zake ikiwa sambamba na usajili na usishangae kusikia Donald Ngoma, Obrey Chirwa na hata Thabani Kamusoko kuondoka Jangwani.

Tayari ameelezwa kuja na kiungo mkabaji, hivyo nafasi ya Kamusoko, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite mmoja wao yupo shakani kukiacha kikosi cha Yanga.

Hata hivyo, Lwandamina aliliambia BINGWA kwamba ameona udhaifu kwa safu ya ushambuliaji na kama atakuja kuinoa timu hiyo ni lazima kuleta straika mkali wa kucheka na nyavu kauli ambayo pia haiwaachi salama Ngoma, Amissi Tambwe na Chirwa.

“Nitahitaji kuwaona wachezaji wote kufanya nao mazoezi na kujua uwezo wa kila mmoja, lakini kwa wale niliobahatika kuwaona uwanjani kupitia video naona udhaifu katika ushambuliaji na pia kiungo hivyo hilo litakuwa suala la kwanza kulifanyia kazi,” alisema Lwandamina.

Ni kawaida kwa kila kocha huamini katika mifumo yake ambayo inaweza kumpa matokeo mazuri hivyo hata kwa Lwandamina lazima atafanya mabadiliko makubwa.

Lwandamina alijiunga na Zesco United, 2014 na ameipa mataji mawili ya Ligi Kuu, Barclay Cup, Charity Shield na ameiongoza timu hiyo 2016 kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -