Saturday, November 28, 2020

NGOMA, TAMBWE WA KWANZA KUONDOKA YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

YANGA wameonyesha kutotaka masihara baada ya kuwatamkia wazi washambuliaji wao wawili, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwamba milango iko wazi wanaweza kuondoka kama wanataka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Paulo Malume, alizungumza na BINGWA jana na kusema kwamba hawatakuwa na kipingamizi kwa nyota yeyote ambaye ataona hafurahishwi na maisha ya Jangwani na kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo.

Alisema katika nafasi ya mshambuliaji wapo mbioni kutafuta mwingine ambaye atakuwa na uwezo wa kucheza katika nafasi hiyo, ikiwamo ya Ngoma ambaye ameonyesha nia ya kutotaka kuongeza mkataba mpya.

“Kumekuwapo na tetesi nyingi juu ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wetu huku wengine wakiwa wamebakisha miezi michache kabla ya mikataba yao kwisha, tunasema ruksa wao kuondoka, hatuwezi kuwazuia wala kuwazibia riziki zao sehemu nyingine,” alisema Malume.

Malume aliongeza kwamba wapo katika mikakati kabambe ya kufanya usajili bab kubwa, baada ya kubaini mapungufu kadhaa katika kikosi chao msimu huu.

“Tutaangalia mshambuliaji mwingine ambaye atakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote uwanjani baada ya kupata ripoti ya kocha msimu ukimalizika,” alisema Malume.

Malume aliwatoa wasiwasi mashabiki wa Yanga na kuwataka kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho wapo mbioni kukifanyia maboresho kikosi chao kuelekea msimu ujao.

“Yanga tuwe watulivu, pesa ipo na tutasajili mchezaji yeyote tunayemtaka, kwa hiyo tutulie japo tumefanya vibaya Ligi ya Mabingwa Afrika tunajipanga kwa Kombe la Shirikisho,” alisisitiza na kuongeza:

“Tunaelekea mechi za kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na kama tukifanikiwa kutinga hatua ya nane bora kuna fedha na tutatumia fedha hizo kwenye usajili na kuboresha kikosi chetu,” alisema Malume.

Nafasi ambazo Yanga wamepanga kuzifanyia maboresho ni ya kipa, beki wa kushoto, mabeki wa kati, kiungo na straika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -