Wednesday, October 28, 2020

NI AZAM YENYE HASIRA NA MAJIMAJI YENYE MACHUNGU LEO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MARTIN MAZUGWA

MARA baada ya kushindwa kutamba kwa mara nyingine dhidi ya African Lyon, Azam FC leo inashuka dimbani ugenini mjini Songea kuikabili Majimaji katika pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji.

Azam ililazimishwa suluhu na African Lyon katika mechi yake iliyopita iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Suluhu hiyo ilikuwa ni mwendelezo wa kukosekana mbabe baina ya timu hizo ambazo katika pambano la mzunguko wa kwanza zilitoka sare ya bao 1-1.

Azam ambayo inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 26 baada ya kushuka uwanjani mara 16, itaikabili Majimaji iliyoko nafasi ya 14 ikiwa na pointi 16 na iliyopoteza mechi yake iliyopita baada ya kulazwa bao 1-0 na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kama Azam itafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo itafikisha pointi 29, hivyo kupunguza pengo kati yake na Simba iliyoko kileleni na pointi zake 38 na Yanga iliyojikita kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 35 kabla ya mchezo wa jana.

Ofisa Habari wa Azam, Japhar Idd, alisema kikosi chao kipo katika hali nzuri kiushindani kuelekea mchezo huo.

“Kikosi kiko vizuri kuikabili Majimaji na kupata ushindi hasa baada ya kocha Zeben kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Lyon,” alisema.

Kuelekea mchezo huo, Iddi alisema  Azam itawakosa nyota wanne ambao wanasumbuliwa na majeraha akiwataja kuwa ni Abdallah Kheri, Mudathir Yahya, Gadiel Michael na Daniel Amouh.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -