Saturday, October 31, 2020

NI BORA KUPENDWA KULIKO KUPENDA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MICHAEL MAURUS,

KARIBUNI sana wasomaji wangu katika safu hii ambayo huwajia kila Jumamosi na Jumanne, ikilenga katika kujuzana hili na lile kuhusiana na mambo ya uhusiano wa kimapenzi.

Kabla ya kuanza kutitirika, nitoe pongezi kwa wasomaji waliojitokeza kuchangia mada ya wiki iliyopita iliyokuwa ikisema: ‘Yupi ni mpenzi bora, anayekupenda au unayempenda?’

Bila kupoteza muda, hebu tuone wasomaji wametoa maoni gani juu ya mada hiyo:

Kwa upande wangu naona bora kupendwa kuliko kupenda, kwa sababu  ukipenda mwisho utakuwa mtumwa wa mapenzi. Samson Mabusi wa Geita.

Naona bora vyote viwe sawa kupendwa  na kupenda, ila unatakiwa kumpenda mtu anayekupenda na katika kupendwa moyo ndio unaamua kumpenda au la, unaweza kupendwa ila usipende. Diego wa Mwanza.

Kupendwa ndio bora kuliko kupenda mwana, mtu unapopendwa ni rahisi na wewe kumpenda yule anayekupenda lakini unapokuwa unapenda ni ngumu moyo wa mwenzio kuubadilisha ukupende na hasa pale unapokuwa haupo moyoni mwake. Baraka wa Ukonga Banana, Dar es Salaam.

Tungekuwa na utamaduni wa kusoma magazeti yenye mada kama hizi zenye mafunzo makubwa katika mahusiano, kusingekuwa na migogoro ya kimapenzi.

Binafsi kati ya kupendwa na kupenda, bora kupendwa kwani unapopendwa, yule anayekupenda anakuwa mnyenyekevu kwako, mbunifu wa mapenzi ili aweze kukuteka, hawezi kuchepuka hali ambayo husaidia kukuepusha na magonjwa yanayoepukika na matokeo yale utajikuta ukiwa na afya njema na kufanya shughuli zako za kimaisha bila presha yoyote. Ukisema uwe ni yule unayempenda wewe, unaweza kujikuta ukibaki kunyanyasika na mwisho wa siku, kupoteza mwelekeo wa kimaisha. Seif Seif wa Hollwood Barber Shop mkabala na kituo cha mafuta cha TSN kilichopo Masasi, Mtwara.

Kupendwa ni bora ndio maana huwa tunasema ukipendwa deka. 0772841558

Ni bora ukapendwa kuliko kupenda utaumiza akili sana. Jeremiah Elias wa Shinyanga.

Mi naona bora kupendwa maana inatokea umempenda mtu kwa dhati mno lakini yeye hakupendi licha ya kuwa naye kimapenzi, lakini atakuwa na wewe kama kukulazimisha tu lakini si kukuonyesha upendo wa kweli kutoka moyoni na mwisho anakuja kukuliza. Nelson Manga wa Mbeya.

Ni bora kukutana wote mnapendana hii itakuwa raha na mtaufurahia uhusiano wenu kuliko kumpenda mtu asiyekupenda tabu na manyanyaso kwako vitakuwa ni vya kawaida. Zedy Breson wa Chalinze.

Bora kupendwa kwasababu mpenzi wako atakufanyia kila kitu unachotaka kwa jinsi anavyoweza asikwambie mtu, kupendwa raha. Fatuma Abdallah wa Mtoni kwa Aziz Ali, Dar es Salaam.

Bora kupendwa kuliko kupenda kwani unaweza kupata manyanyaso sana katika mapenzi. Joseph Ngesela.

Kupendwa ni bora sana kuliko kupenda, ila kunatakiwa kuwapo na angalizo kwani inaweza kutokea akupendae hisia zako haziko kwake, hivyo badala ya furaha hugeuka huzuni. Cosmas wa Same, Kilimanjaro.

Huwezi kumpenda asiyekupenda, lazima wote mpendane hapo mambo yatakuwa sawa.0714 399566

Bora kupendwa ni raha kuliko kupenda. Michael Mrema wa Geita.

Ni bora anayekupenda maana atakuwa pamoja na wewe katika maisha. Samwel Kalolo wa Magereza, Morogoro.

Mimi naona bora kupendwa kuliko kupenda. Khamis wa Songosongo, Kilwa.

Bora kupendwa kuliko kupenda. Matrida Simon wa Njombe.

Ni bora kupendwa. Nilikuwa na mpenzi wangu nampenda sana ila yeye hanipendi kwa dhati. Nifanyeje jamani? Jeremiah Mozes wa Sengerema, Mwanza anapatikana kwa simu namba 0752025920.

Kupenda ni bora lakini kupendwa ni bora zaidi kwasababu kuna nafasi kubwa ya kufurahia penzi. Kuulazimisha moyo kumpenda mtu asiyependa ni matatizo. Muyuga wa Bunda.

Bora zaidi ni kupendwa naweza kusema hivyo kwasababu itakupa ufanisi mkubwa wa kupata kila unachotaka kutoka kwake na pia itaupa moyo wako nafasi kubwa ya kutojutia hata kama aliyekupenda itatokea akakuacha, lakini ukipenda utakuwa muda wote moyo wako una wasi wasi juu ya unayempenda na ikitokea akawa hakupendi jinsi unavyompenda, unaweza kufanya kitu ambacho siyo kizuri, mfano kujiua lakini kama unapendwa, moyo wako utakuwa na furaha muda wote. Simon Akyoo wa Arusha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -