Wednesday, October 28, 2020

Ni hatari kubwa mpenzi wako kuamini kuwa humpendi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KILA binadamu kwa namna yake hujiona yeye ni bora zaidi. Yeyote unayemuona mtaani kwa namna yoyote alivyo kuna mahali hujiona yeye ni bora zaidi. Hii tabia ndiyo humfanya binadamu awe na furaha na kujiona anastahili sana kuishi.

Binadamu anayetokwa na sifa hii, ama kwa kufanywa kuamini au kwa kujifanya kuamini kuwa yeye si bora, hupoteza furaha ya maisha na hatimaye huchukua uamuzi mgumu (mbaya) katika maisha yake. Huwa kama si kujiua, basi huamua kuwa binadamu katili.

Tathimini inaonesha watu wengi wanaochukua uamuzi wa kukatisha maisha yao, huwa na hisia za kujiona wao si bora kwa wenzao, hivyo wanaona dunia haina tena maana katika maisha yako.

Katika dunia ya mapenzi hali hii ina sura mbili. Mosi, mtu akioneshwa kuwa yeye si muhimu katika maisha ya anayempenda, mwenye uwezo wa udhibiti wa hisia zake atajitahidi kuwa na mhusika, ila baadaye ni lazima ataachana naye kama mhusika hatabadilika mapema. Wengine ni kama wale tunaosikia katika vyombo vya habari kuwa walichukua uamuzi mbaya, ama wa kujiua au kumdhuru mhusika.

Uko vipi katika mahusiano yako? Unampenda mwenza wako mpaka anajua kuwa unampenda? Ama unampenda huku mwenzako akiwa na viulizo vingi juu ya mapenzi yako?

Kuna hatari sana mpenzi wako kuamini kuwa humpendi. Hatari zenyewe ni kama zifuatazo: Mpenzi wako akiwa anaamini kuwa humpendi, hawezi kujitoa kwa kiwango kikubwa siku zote katika maisha yake. Ajitolee vipi wakati anaamini kuwa wewe si mtu unayempenda, hivyo muda wowote unaweza kumtema?

Pia, mtu mwenye mashaka juu ya upendo wako kwake, hawezi kuhisi hatia yoyote pindi anapokukosea. Sasa hapa hatari yake huegama zaidi katika usaliti na heshima juu yako. Mtu huyu hata akitongozwa ama kutaka kuanzisha mahusiano na mtu mwingine huwa hahisi kuwa kutekeleza wazo lake ni vibaya kwa sababu anajua kuwa wewe humpendi, hivyo utamuacha. Na kwa maana hiyo,  hata yeye kuanzisha mahusiano mengine huku yuko na wewe anaona kama anaandaa mazingira ya kukuhama salama.

Una hakika mpenzi wako anajua kuwa unampenda? Hakikisha maneno na matendo yako yote yanachora picha ya upendo wako juu yake. Bila kuonesha kuwa unampenda sana mpenzi wako, usitegemee sana uaminifu wake juu yako. Uaminifu wa mpenzi wako unategemea sana namna anavyouhisi upendo wako juu yake.

Akiwa anauhisi vikubwa upendo wako, huenda atajiuliza hivi, mbali na mapenzi haya, thamani hii, kwanini nimsaliti huyu mtu? Je, akijua mimi nitakuwa katika hali gani? Si ataniacha, na akiniacha nitampata nani mwenye mapenzi ya kweli na mwenye kujali kama huyu? Kwa fikra hizi katika kichwa chake, hatimaye hujiona mzito kuchukua uamuzi wowote muovu dhidi yako.

Ila hali huwa tofauti sana pale unapokuwa uko naye ilimradi. Yaani ni kama unampenda au humpendi. Uko naye tu bila kumfanya aone kuwa yeye ni mtu muhimu na wa thamani katika maisha yako. Katika hali hii akitokewa na mtego wa usaliti huwa na mawazo yasiojali sana upande wako. Atajiuliza tu yule hanijali na kunithamini huenda kwa sababu ana mtu mwingine. Sasa vipi nisiwe na mtu mwingine wakati yeye anaonekana kuwa naye? Hapo ndipo anawaza kuwa huenda huyu anayeongea naye anaweza kuwa mtu mwenye kujali na kuthamini zaidi.

Mara akiwa katika mawazo ya namna hiyo anajikuta anafanya uamuzi wa usaliti juu yako kwa kuamini kuwa hata wewe unamfanya si lolote kwa sababu una mtu mwingine unayemuona wa thamani na maana zaidi katika maisha yako.

Kutomuonesha mwenzako kuwa unampenda si njia ya kudumisha mahusiano yako kama imani ya wengi ilivyo, ila ni njia ya kuyapeleka mahusiano yako gizani zaidi. Hakuna binadamu ambaye hapendi kujua na kuoneshwa kuwa anapendwa na kuthaminiwa.

Uimara wa uhusiano wowote, ni hali ya kuoneshana kupendana na kuthaminiana. Bila hali hii hakuna amani wala furaha. Hakuna mtu ambaye hupenda kujiona kuwa yeye ni wa ziada kwa mwenzake. Kila mmoja kwa nafasi yake hupenda kujiona ana thamani na ni muhimu sana katika maisha ya mwenzake.

Katika hali hii ndiyo maana kila muda mpenzi wako anaweza kukuuliza unanipenda kwa asilimia ngapi. Swali hili si la kipumbavu hata kidogo. Wengi wanauliza hivi kutaka kutakasa nafsi zao kwa furaha.

Kila mwanamke anataka kuwa malkia kwa mwanamume wake, na kila mwanamume anataka kuwa mfalme kwa mwanamke wake. Ila hali hii huwa miujiza mtu akihisi kama humjali, humsikilizi na unampa maneno ya mashaka juu ya nafasi yake katika maisha yako.

Ili mahusiano yako yaongeze maana, inabidi mwenzako ajue kuwa unampenda sana. Akijua unampenda sana, unakuwa umempa mtihani mkubwa  wa kisaikolojia. Kila wakati akitaka kufanya ujinga na kukumbuka upendo wako juu yake, atasutwa na nafsi yake na mwishowe ataendelea kubaki mtiifu kwako.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -